Breaking News

EZY AUTOMOTORS YAWEKA NJIA RAHISI ZA UNUNUZI WA MAGARI

Kampuni ya EZY Automotors imesema inaendelea kuwawezesha Watanzania kupata magari kwa njia mbalimbali za malipo, ikiwemo ununuzi wa fedha taslimu, mikopo pamoja na mpango wa kuweka fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kununua gari.

Akizungumza katika Maonyesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Geita Mkurugenzi wa EZY Automotors Samuel Nyoni, alisema kampuni hiyo imeweka mifumo inayolenga kumwezesha mteja kuagiza gari analolihitaji kwa kuzingatia bajeti yake.

Aidha mteja anayenunua gari kwa fedha taslimu huchagua gari analolihitaji kufanya malipo na kukabidhiwa gari lake, huku kampuni ikihakikisha mchakato wa uagizaji na usafirishaji unafanyika kwa usalama.

“Tunataka kuhakikisha mteja anaagiza kupitia EZY Automotors akiwa na uhakika kwamba fedha yake iko salama na gari lake litamfikia salama,” alisema Nyoni.

Kupitia kwa wateja wanaohitaji kununua magari kwa njia ya mkopo, kampuni imeweka utaratibu unaozingatia sifa za mwombaji, ikiwemo kuwa ameajiriwa au ni mfanyabiashara.

Nyoni aliongeza kuwa kampuni hiyo pia ina mpango wa uwekezaji unaomruhusu mteja anayetarajia kununua gari baadaye kuanza kuweka fedha kidogo kidogo hadi kufikia kiwango kinachomwezesha kuchagua na kununua gari analolihitaji.

“Kwa mteja ambaye ana malengo ya kununua gari miezi au miaka ijayo, tunampatia akaunti maalumu ambapo anaweza kuwekeza fedha kidogo kidogo. Fedha ikitimia, anakuja kuchagua gari analolihitaji na tunamkabidhi,” alisema nyoni

Aidha EZY Automotors inatoa fursa kwa wateja kupata uchaguzi mpana wa magari, tofauti na mfumo wa kwenda sehemu moja na kukuta magari machache yaliyopo tayari.

“Ukiwa EZY Automotors unaweza kupata uchaguzi mpana zaidi. Inawezekana sehemu nyingine ukaenda ukaona magari mawili au matatu, lakini kupitia EZY Automotors utaweza kuchagua gari unalotaka na sisi tutaleta gari ambalo umeagiza,” alisema Nyoni.

Vilevile kampuni hiyo huzingatia uwezo wa kifedha wa mteja katika mchakato wa uagizaji wa gari, ili kuhakikisha anapata gari linaloendana na bajeti yake.