WATAHINIWA 667,040 KUANZA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE LEO
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Profesa Saidi Ally Mohamed, amesema watahiniwa 667,040 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) mwaka 2026, utakaofanyika kuanzia leo Oktoba 19 hadi Novemba 6 katika shule za sekondari 6, 265 na vituo 802 vya watahiniwa wa kujitegemea nchini.
Kati ya watahiniwa hao, 644,085 ni wa shule, wakiwemo wavulana 297,309 na wasichana 346,776. Watahiniwa 22,955 ni wa kujitegemea, wakiwemo wanaume 10,223 na wanawake 12,732.
Aidha, watahiniwa 983 wenye mahitaji maalumu wamesajiliwa, wakiwemo 910 wa shule na 73 wa kujitegemea. Mahitaji yao yanajumuisha uoni hafifu, kutokuona, uziwi, ulemavu wa akili na ulemavu wa viungo.
NECTA imesema idadi ya watahiniwa wa shule imeongezeka kwa 74,202, sawa na asilimia 13.02, ikilinganishwa na watahiniwa 569,883 waliosajiliwa mwaka 2025.
Aidha, ratiba ya mtihani huo imefanyiwa marekebisho kwa kuzingatia tahadhari ya mvua za El Niño. Watahiniwa watakaoshindwa kufanya mtihani kutokana na changamoto zitakazosababishwa na mvua hizo watapewa nafasi nyingine ya kufanya mtihani katika kipindi maalumu kitakachopangwa.




