KIWANGO CHA MAUZO KATIKA SOKO LA HISA (DSE) CHA SHUKA.
KIWANGO
cha Mauzo ya hisa katika Soko la hisa Dar es Salaam kimeshuka Kutoka shilingi
bilioni 11.6 ikilinganishwa na shilingi bilioni 5.6 cha wiki iliyopita hali iliyochangiwa kupanda kwa Sekta ya viwanda kwa asilimia 11.47 baada ya hisa
TCCL Kupanda kwa asilimia 0.61 .
Akizungumza
na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam
Afisa Mwandamizi wa Soko la hisa Dar es salaam (DSE) Bi, Mary Kinabo
amesema kiwango cha mauzo kimeshuka imesababishwa na kupanda kwa mauzo ya hisa
katika sekta ya viwanda kwa asilimia 11.47 kufuatia bei ya hisa za hisaTCCL
naTBL kupanda kwa asilimia 0.61 Sekta ya
huduma za kibenki na kifedha imeonekana ikipanda kwa 5.83baada yahisa zilizo
kwenye kaunta katika soko hilo kupanda .
Amesema
ya Idadi ya mauzo imeshuka kwa 49% na kufikia TZS 5.9 Bilioni kutoka TZS 11.6
Bilioni, uku Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kiwango chake kimepanda
mara 3 zaidi hadi kufikia Milioni 5.4 kutoka Milioni 1.7.
Aidha
Bi Kinabo amezitaja kampuni tatu juma
hili zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kuwa ni DSE kwa
asilimia 61%, CRDB kwa asilimia 35%, TBL kwa asilimia 2.6%.
Katika hatua nyingine bi Kinabo amesema Shindano
la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (DSE Scholar Investment
Challenge 2016) ambalo litafikia tamati terehe 2 August 2016 limeendelea
kuonyesha mwamko mkubwa kwa wanafunzi kutoka vyuo hivyo na kuvitaja vyuo ambavyo
vimeingia tano bora ni Chuo Cha Biashara (CBE), kinaongoza kikifatiwa na chuo
cha .Institute of Rural Development Planning (IRDP),
Amevitaja vingine kuwa ni University of Dodoma (UDOM), Institute of
Accounts Arusha (IAA), Sokoine University of Agriculture (SUA).




