Mwanamuziki wa Kimataifa
wa Miondoko ya Dansi kutoka Nchini Congo, Antoine Christophe Agbepa Mumba
maarufu kama “Koffi Olomide” amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela baada ya
kuonekana na hatia ya kumdhalilisha kwa kumpiga dansa wake wakati wakiwasili
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nchini Kenya hivi
karibini.
Mwanamuziki huyo alikamatwa mapema leo akiwa
nyumbani kwake katika mji wa Kinshasa na kupelekwa Mahakamani moja kwa moja na
kukutwa na hatia hiyo.
Hukumu hiyo imetolewa baada ya ushahidi huo
kuonekana akimpiga dansa wake na atatakiwa kuitumikia adhabu hiyo kwani
hajapewa nafasi ya kulipa faini ya aina yoyote ile.
hatua ya kumkamata Mwanamuziki huyo ilifikiwa
baada ya kuanzishwa kwa kampeni ya baadhi ya wadau wa maswala ya kijamii
wakiongozwa na Zakarie Bababaswe aliyefungua kesi kwa niaba ya Serikali ikiwa
ni madai ya udhalilishaji kwa dansa wake, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya
Kongo, kuamua kukamatwa kwake na kusema anataka haki itendeke.
KOFFI OLOMIDE AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 18 BAADA YA KUKUTWA NA HATIA YA KUMDHALILISHA DANSA WAKE
Reviewed by Harakati za jiji
on
July 26, 2016
Rating: 5