Breaking News

UTAFITI: ASILIMIA 80 YA WAFANYAKAZI WANAFANYAKAZI BILA MIKATABA RASMI HASA KATIKA SEKTA YA UCHUKUZI NA HABARI



Mgeni rasmi Mkurugezi wa wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji bw Alfred Mapunda akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya haki za binadamu katika biashara ya mwaka 2015 jijini dar es salaam.
Mtafiti wa ripoti hiyo kutoka kituo cha sheria na haki za binadam (LHRC), Clarence Kipobota akiwasilisha mada kuhusu ripoti ya haki za binadam katika biashara ya mwaka 2015 jijini dar es salaam.

Mkurugenzi wa  kituo cha sheria na haki za binadamu (LHCR) bi Hellen Kijo Bisimba akifafanua jambo katika uzinduzi wa ripoti ya haki za binadam katika biashara ya mwaka 2015 jijini dar es salaam.



Wadau kutoka taasisi za umma, mashirika yasiyo ya kiserikali, mabalozi, waandshi wa habari wakipewa nakala za Ripoti ya haki za binadam katika biashara ya mwaka 2015 jijini dar es salaam. 

Washiriki wa uzinduzi hiyo katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 
                                            Frank Wandiba-Dar es salaam
Serikali imesema inatambua mchango mkubwa wa wadau mbalimbali hasa kuwa mstari wa mbele katika  kuelimisha jamii kuzitambua na kuzitatua changamoto zinazowakabili katika sekta mbalimbali hususani maswala ya haki za binadamu pamoja na tatizo la ajira za utotoni.



Akizungumza  mara baada ya kuzindua ripoti hiyo kwa niaba ya waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Mkurugezi wa wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji bw Alfred Mapunda alisema  serikali  inatambua changamoto zilizopo na inaendelea kuhimiza wadau mbalimbali kushirikiana na serikali ili kumaliza  changamoto hizo kwa kuwataka wafanyakazi wasiokuwa na vyama  vya wafanyakazi kuunda vyama  hivyo ili kutetea maslahi  yao.



Mapema akiwasilisha taarifa ya ripoti hiyo mtafiti wa ripoti hiyo kutoka kituo cha sheria na haki za binadam ( LHRC), Clarence Kipobota amesema zaidi ya watoto  million 5  wenyenye  umri chini ya miaka 18  sawa na asilimia  84  wamebainika  kufanyishwa kazi  katika  maeneo mbalimbali hapa nchini  ikiwemo mashambani.



Amesema ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wafanyakazi waliofikiwa na kuhojiwa wamebainisha kufanya kazi bila mikataba rasmi wengine kuwa na mikataba  mibovu  hasa katika  sekta ya uchukuzi pamoja na sekta ya habari.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa  kituo cha sheria na haki za binadamu (LHCR) bi Hellen Kijo Bisimba, amesema uandaaji wa ripoti hiyo ulijikita zaidi katika mambo muhimu ikiwemo Ardhi.



Amesema wanachi wengi waliojiwa wakati wa utafiti walisema kuwa ardhi yao imekuwa ikitwaliwa na wawekezaji bila kulipwa fidia stahiki jambo ambalo limekuwa likipelekea kusababisha migogoro.


Aidha bi Bisimba ameongeza kuwa ripoti hiyo iliangalia pia maswala ya ukatili wa kijinsia pamoja na masuala ya ukusanyaji mapato pamoja na kuwepo kwa misamaha mingi ya kodi kwa wawekezaji