PROF MBARAWA KUZINDUA TRENI YA PUGU KESHO
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa ratiba ya
uzinduzi wa huduma mpya ya usafiri wa reli Jijini kwenda Pugu nakuonesha kuwa
utafanywa na Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
saa 9 mchana hapo kesho katika kituo kikuu cha Reli cha Dar es Salaam.
Ratiba hiyo inaonesha baadhi ya waalikwa kuwa ni Viongozi
waandamizi wa Serikali kutoka Ofiasi ya Mkuu wa Mkoa na Jiji pamoja na wadau
muhimu katika sekta ndogo ya usafirishaji wa Reli nchini.
Huduma ya treni ya Pugu ilianza kwa majaribio tokea Agosti 01,
2016 ambapo ilipokolewa vizuri na Wakazi wa Vingunguti, Banana, Gongo la Mboto
na Pugu Majohe na kwamba changamoto iliowakuta Viongozi wa TRL ni kudhihirika
kuwa mabehewa 10 ya treni hiyo hayakidhi wingi wa abiria njia hiyo.Hata hivyo kwa takriban wiki moja treni hiyo ilikuwa ikitoa huduma zake za awamu mbili za asubuhi na jioni bila ya kutoza malipo yeyote.
Huduma za kuanzia kesho zitaanza na tozo ya Shilingi 400 kama ilivyo kwa treni ya Ubungo Maziwa ikisubiri nauli halisi baada ya kukamilika mchakato wa ukokotoaji ambao unasimamiwa na Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra) ambao umepangwa kuanza Agosti 11, 2016.
Imetolewa
na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Masanja Kungu Kadogosa,
Dar es Salaam,
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Masanja Kungu Kadogosa,
Dar es Salaam,






