Brunei: Nchi Yenye Utawala Wa Kustaajabisha Zaidi Duniani.
1. Brunei ukipenda iite 'Darusalaam' ama nyumba ya amani ni nchi
ambayo raia wake hawalipi kodi YEYOTE. Hata maisha ya wananchi wake ni mazuri
na mshahara wa chini kabisa ni dola 25 kwa saa (Tshs 50,000), huku ukosefu wa
ajira ukiwa ni wastani wa 5% tu.
Serikali inalipa gharama zote
muhimu, mpaka chakula kinalipiwa ruzuku. ukifanya kazi kule hakuna income tax
(There is no personal income tax or capital gains
tax). Sultani anasimamia vizuri sana export ya mafuta na gesi.
GDP
ya Brunei imepanda hadi 56% kuwa nchi ya tano duniani (16.11 billion USD in
2013) na IMF wanasema nchi hiyo haidaiwi HATA shilingi MIA.
2. Sultan wa Brunei Mohammad Hassan Bolkiah ndiye Raisi tajiri
kuliko maraisi wote duniani, Maarufu kwa utumiaji wa dhahabu kwa kila kitu,
hali ila na vijiko vya dhahabu, na nguo anazo vaa zimepambwa kwa dhahabu na
fedha. Huyu anamiliki Jumla ya MAGARI 5000 YA KIFAHARI (tazama kasri na moja ya
gari lake lake la dhahabu tupu pichani).
Sultan huyu anamiliki pia ndege aina ya Boing 747 thamani yake
ikiwa ni dola milion 100 ambamo pia nakshi pekee ni dola milioni 120 humo
utakuta vyoo na vyumba vya dhahabu, pia anamiliki ndege ndogo sita na helicopta
moja. Arusi ya mtoto wa Sultan wa Brunei ilifanyika kwa muda wa siku 14 kwa
gharama ya 5 milion dolla huku watu wote walioalikwa wakila na kunywa na
kusaza, na kuhudhuriwa na zaidi ya maraisi 25.
3. Elimu ni Bure kabisa na watoto chini ya miaka 12 HUTIBIWA
BURE huku watu wazima wakilipia dola 1 tu kwa Matibabu. Kadhalika ukioa tu
unapewa na gari. Ni nchi mojawapo ambayo ina uwiano mkubwa wa watu na magari
(1:209)-Ikiwa hakuna tiba ya ugonjwa wako Brunei unapelekwa nje ya nchi hasa
Malaysia na Singapore kwa gharama za serikali.
4. Pombe imepigwa marufuku kabisa kisiwani Brunei ingawa wageni
wanaweza kuagiza kiwango chenye ukomo na Hakuna NGURUWE hata mmoja nchi nzima.
5. Ukiwa Brunei marufuku kupoint kutumia kidole cha shahada
kuonesha kitu. Kidole gumba tu hutumika kupoint kitu na ni Lazima kuvua viatu
unapoingia nyumba yeyote ndani ya Brunei.
6. Hii inatumia mfumo wa SHERIA ambapo 'Wezi hukatwa mikono na
wazinifu kupigwa mawe'. Mwaka 2014 ilipitisha sheria ya kupigwa kwa mawe hadi
kufa yeyote atakayebainika anafanya USHOGA (Homosexual) lakini kwa uthibitisho
wa mashahidi WANNE.....Unaweza kusherehekea Noeli (X-mass) lakini si kwa kuweka
mapambo yake kama vilemti wa Xmass nk.
7. Ingawa Kisiwa cha Brunei Kina BUNGE lakini nchi hiyo HAINA
Uchaguzi, Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 1962, kuna chombo kimoja tu cha
habari kinachomilikiwa na Serikali, ni aghalabu sana kwa media kuipinga
serikali
8. 93% ya watu wote Wameenda Shule kwa kiwango cha DEGREE.







