Kutoka RuKwa: Auawa Kwa Kupigwa Na Ndugu, Wakimtuhumu Kuaibisha Ukoo Kwa Madeni

Mkazi wa kijiji cha Kafukoka kata ya
Kisumba wilayani Kalambo mkoani Rukwa Kalasto Katanti (40) ameuawa kwa kupigwa
na ndugu zake wakidai kuchukizwa na madeni aliyonayo kwamba anaaibisha ukoo.
Tukio hilo limetokea Januari 1,2018
majira ya saa 1:30 usiku.
Inaelezwa kuwa kabla ya kuuawa kwa
kipigo hicho,Katanti alikuwa anadaiwa shilingi 64,000/= deni ambalo lilikuwa ni
la muda mrefu kiasi ambacho alionekana ameshindwa kulilipa.
Akizungumzia tukio hilo katibu tawala
wa wilaya hiyo Frank Sichalwe aliiambia Malunde1 blog kutokana na deni hilo
ndipo ndugu zake wawili ambao ni Florence Zunda (38) na Dafusi Zunda(35)
walipoamua kumpiga hadi kumuua wakidai kuwa wamechoshwa na tabia yake ya kukopa
fedha wakati anajua hana uwezo wa kulipa kitendo kinachodhalilisha ukoo
wao.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa George
Kyando amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kuongeza kuwa watuhumiwa wa
mauaji hayo wanashikiliwa na polisi na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Kamanda Kyando alionya tabia ya wananchi
kujichukulia sheria mkononi kwani vitendo hivyo vimekuwa vikisababisha mauaji
ya watu hovyo na kuwataka wanapokuwa na matatizo ni vizuri wakatumia njia ya
mazungumzo kufikia muafaka.
Na Walter Mguluchuma



