Mbowe : Mollel Ni Daktari Asiye Na Uwezo...Mwanaume Anajikomba Komba Kwa Watu Wa Ccm
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman
Mbowe amefunguka na kukanusha taarifa alizotoa mgombea Ubunge wa CCM jimbo la
Siha, Dkt Mollel kuwa aliamua kuhama CHADEMA na kwenda CCM kwa kuwa alizuiwa
kuongea na viongozi wa CHADEMA.
Mbowe amesema hayo leo katika uzinduzi
wa kampeni za mgombea Ubunge wa CHADEMA katika jimbo la Siha, Elvis Mosi na
kudai kuwa Moller hakuwa na uwezo wa kujenga hoja na ni mtu ambaye amekuwa
akijikomba kwa watu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Mollel
hajazuiliwa na mtu bali ni Dk. asiye na uwezo, hana uwezo wa kujenga hoja ni
mwanaume anajikomba komba kwa watu wa CCM, niwambie watu wangu wa Siha
mnapokuwa mnachagua viongozi sisi kama chama tunawapima kila mwaka, huyu
uchaguzi unaokuja ataturudishia jimbo au atatunyima jimbo? Na kwa vigezo
mbalimbali vya chama vilivyofanyika wananchi wa Siha mshukuru kwa sababu
mlikuwa unatuchagulia gunia la misumari bila kujua, angebaki kwa miaka mingine
mitatu kwenye nafasi yake ya Ubunge CHADEMA wananchi wa Siha
mngeichukia" alisema Mbowe.
Mbowe aliendelea kusisitiza kuwa
kitendo cha Mollel kujivua uanachama na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge jimbo
la Siha ni mpango wa Mungu na ni jambo zuri kwani lingefanya chama hicho
kuchukiwa na wananchi.
"Huu
ni mpango wa Mungu aliona wananchi wa Siha nikiwaachia hili gunia la misumari
litakuwa si jambo zuri hivyo akamtia uchizi akaamua kuhama chama, kwa hiyo
hatuna cha kulia kila kitu ni mpango wa Mungu, alijua kwamba Siha tumejitwisha
gunia la misumari",alisema Mbowe.
Chanzo-
EATV



