Baada Ya Kuifungua CAMON CM
Ni ukweli usiopingika
kuwa TECNO, ni kampuni inayoendelea kufanya vyema katika uzalishaji na uuzaji
wasimu janja barani Afrika hivi karibuni wamepokea mtazamo chanya kupitia toleo
lao jipya Camon CM lenye sifa ya kuwa na kioo chenye wigo mpana.
Ufuatao
ni uchambuzi baada ya kuifungua Camon CM
Camon
CM imehifadhiwa vema kwenye kasha lenye sildi, ndani ya boksi nilikutana na
chaji, vinasa sauti [earphone], lakini pia simu ina ulinzi wa kioo [screen
protector],sambamba na kitabu kinachotoa maelezo kuhusu mipangilio ya simu na
matumizi yake
Uwiano wa 18:9 ndo kitu
kilichonivutia zaidi ambavyo nilikuwa natamani nipate simu yenye wigo mpana
eneo la kioo,TECNO wameliwezesha hilo, ambapo Camon CM ina skrini yenye ukubwa
wa inchi 5.7 ambapo niliweza kutazama filamu na kusoma habari mitandaoni
kwa kuji nafasi pasipo kuwa na mipaka ya kuta za simu.
Nilijipiga picha
[selfie] zikatoka na ubora wa HD, kupitia 13 MP mbele na nyuma ikiambatana na
flashi zake 4 ambazo hutoa mwanga kwa kuwaka waka simu inapoita hivyo ni
rahisi kugundua simu ikiita hata ikiwa umetoa muito.
Nimehifadhi
programu zaidi ya 80 nikiwa na 2GB RAM & 16 GB ROM na bado nna nafasi
ya kuweka memori kadi ya ziada kufikia GB 128, hivyo sina tena wasi wasi wa
simu yangu kuzidiwa uwezo kwa kutokuwa na nafasi ya kuhhifadhi kumbkumbu na
programu mbalimbali.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.tecnomobile.com/tz



