Kampuni Ya Simu Ya TECNO Yametoa Rasmi Simu Mpya Aina Ya Camon Cm
Kampuni ya
simu za mikononi ikiwa chini ya kampuni mama ya TRANSSION HOLDINGS iliyopo
China, imeachilia rasmi simu janja “smartphone” mpya yenye kioo kamili/enea au
kwa lugha ya kiingereza (Full DISPLAY) yenye ukubwa wa uwiano “ratio” 18:9.
TECNO CAMON CM ni simu mpya kabisa kwa mwaka 2018.
Mambo mengi
yanatarajiwa na wadau kutoka katika simu hii mpya “CAMON CM” kwani ni
muendelezo wa toleo lililopita la CAMON.
CAMON CM inabeba sifa kuu kubwa
ambayo ni kua na kioo enea/kamili “FULL DISPLAY” chenye uwiano wa 18:9,
kuifanya simu hii kua ya kwanza kutoka TECNO ambayo kioo chake hakina mipaka au
mikato kulinganisha na simu zingine zenye ukubwa wa 16:9.
Pia simu
ina urefu wa nchi 5’7 ambayo itamuwezesha mtumiaji kutazama video, kucheza
michezo “Games”, kuperuzi mitandao kwa raha zaidi kulinganisha na simu ambazo
zina mipaka.
Vigezo vingine ambavyo
vinapatikana kwenye CAMON CM ni pamoja na kamera bomba yenye uwezo wa 13MP
kamera ya mbele na nyuma,4G LTE, RAM 2GB, ROM 16GB, na betri yenye ukubwa wa
3000 mAh (Isiyotoka).
Simu hii ina rangi tatu ambazo ni “CITY BLUE”, MIDNIGHT BLACK na
“CHAMPAGNE GOLD
CAMON CM sasa inapatikana,kwa taarifa zaidi tembelea
http//www.tecno-mobile.com/tz



