Siku Ya Wapendanao (Valentine) Ilivyonogeshwa Na Startimes
Kampuni ya Star Media (T) Ltd inayomiliki chapa ya StarTimes,jana katika Siku ya wapendanao iliwapatia fursa wateja wao kupata chakula cha jioni na wapenzi wao katika mgahawa wa kifahari wa Akemi, Posta jijini Dar es Salaam.
StarTimes
ambayo kwa wiki kadhaa iliwapatia nafasi wateja wake kupitia kurasa zake za mitandao
ya Kijamii kutuma picha wakiwa na wapenzi wao ili kujipatia nafasi hiyo adhimu ya
kupata chakula cha jioni pamoja.
Katika
picha zote zilizotumwa na wateja wa StarTimes katika kurasa zao za mitandao ya kijamii,watano
walibahatika kuchaguliwa na baadaye walipatiwa taarifa jinsi ya kufika kwenye mgahawa
kwa ajili ya zawadi maalum.
Kabla ya
kupelekwa mgahawani wapenzi hao walipata nafasi ya kutembelea ofisi za makao makuu
ya Star Media (T)Ltd zilizopo Bamaga, Barabara ya Bagamoyo, Dar es Salaam,
nakujionea jinsia mbavyo StarTimes hufanya kazi kila siku, miongoni mwa ofisi walizotembelea
ni kituo cha Simu (Call Centre), Chumba cha Kurushia matangazo na Duka la vifaa
mbalimbali vya StarTimes.
Wapendanao
hao baadaye walipelekwa mgahawani kwa ajili ya Chakula cha jioni. Yote ikigharimiwa
na kampuni ya StarTimes katika kuonyesha upendo kwa wateja wake katika Siku ya Wapendanao.



