Balozi Wa Sweeden Afungua Maonesho Ya Picha.
Balozi Wa Sweeden
Nchini,Bi. Katarina Rangnitt Akizungumza katika halfa ya ufunguzi wa Maonyesho
Ya Picha Yanayoonesha Jinsi Wazazi Wa Kiume Wa Tanzania Na Sweeden
Wanavyoshiriki Katika Malezi Ya Mtoto, Coco Beach Jijini Dar Es Salaam.
Dar es salaam:
Balozi Wa Sweeden Nchini Bi.Katarina
Rangnitt Amefungua Maonesho Ya Picha Yanayoonesha Jinsi Wazazi Wa Kiume Wa
Tanzania Na Uturuki Wanavyoshiriki Katika Malezi Ya Watoto.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi Huo Jijini Dar Es Salaam, Bi.
Rangnitt Alisema Lengo La Maonesho Hayo Ni Kuonesha Umuhimu Wa Wanaume Kushiiki
Katika Malezi Ya Mtoto Na Kuhamasisha Usawa Wa Kijinsia.
“Ushiriki Wa Mwanaume Kama Baba Kwenye Malezi Ya Mtoto Unaumuhimu
Mkubwa Kwenye Maisha Ya Wanawake, Lakini Pia Unaleta Matokeo Chanya Kwa Wanaume
Wenyewe,” Amesema Bi. Rangnitt.
Alisema Sweeden ni moja ya nchi ambayo imepigwa Hatua Kubwa duniani
Katika Ushiriki malezi ya watoto Kwani Wanaume wamekuwa wakipewa Hata Likizo Ya
Uzazi Pale Wake Zao Wanapojifungua.
Aidha Bi. Rangnitt aliongeza kuwa Baba Anapokuwa Karibu Na Familia
Kabla, Na Baada Ya Mtoto Kuzaliwa Inasaidia Kuwa Na Matokeo Chanya Katika Afya
Ya Mama Na Mtoto, Mama Na Mtoto Hupata Msaada Wa Muda Mrefu Katika Huduma
Mbalimbali, Lakini Pia Na Kuwa Na Mchango Chanya Katika Makuzi Ya
Mtoto Kiafya Na Kiakili.
Maonesho Hayo Ni Ya Siku Sita Na Kilele Chake Ni Machi 21, 2018.
Baaadhi Ya Wazazi Walioshiriki Katika Uzinduzi Huo
Akiwemo Msanii Wa Filamu Za Kitanzania 'Bongo Movie' Singo Mtambalike (Wapili
Kutoka Kushoto) Wakielezea Jinsi Wanavyoshiriki Katika Malezi Ya Watoto Kwenye
Familia Zao.
Baadhi
Ya Watu Waliohudhuria katika halfa hiyo ya uzinduzi Burudani
Baadhi Ya Watu Waliohudhuria katika halfa hiyo ya uzinduzi
wakibadilishana mawazo
Burudani zilikuwepo pia katika uzinduzi huo kutoka katika vikundi
mbalimbali vya jijini dar es salaam.












