CUF Wilaya Ya Kinondoni Yawatumbua Viongozi Wa Kata Ya Tandale Na Makumbusho Kwa Tuhuma Za Usaliti..
Chama cha wananchi CUF wilaya ya kinondoni kimewafukuza waliokuwa viongozi wa chama hicho katika kata ya tandale na kata ya makumbusho jijini dar es salaam kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni za uchaguzi wa marudio wa ubunge jimbo kinondoni.
Akizungumza katika
ofisi ya chama hicho wilaya ya kinondoni jijini dar es salaam katibu wa CUF
wilaya ya kindondoni Bw. Mohamed Mkandu amewataja vingozi hao kuwa ni aliyekuwa
mwenyekiti wa chama hicho kata ya tandale Blandino Mwasabwite na katibu wake
bw. Ally mtumweni.
Amewataja wengne
kuwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho kata ya makumbusho Bi. Pamela Farahani,
mwenyekiti wa tawi la mwanayamala Mashaka Adamu pamoja na mweka hazina wa chama
wa kata hiyo Bw. Halidi Magwai.
Wengine ni mweka
hazina tawi la mchangani, kata ya kigogo waliondolewa ni katibu katibu Sungura,
kata ya Ndugumbi ni Bw Seif ambaye alikuwa Katibu, kata ya magomeni ni
mwenyekiti pamoja na katibu wa chama hicho wameondolewa katika nafasi zao.
“katika kampeni za
uchaguzi wa marudio wa ubunge jimbo la kinondoni viongozi hao wa matawi na
wilaya walikisaliti chama kwa kumfanyia mgombea wa chama cha democrasia na
maendeleo (CHADEMA) bw. Salum Mwalimu kinyume na taratibu wa chama hicho”
alisema Bw Mkandu.
Katika hatua
nyingine Bw. Mkandu amelaani kitendo cha katibu mkuu wa chama hicho Maalim seif
kufanya kongamano katiba kata ya Tandale kwa kile alichokieleza kuwa kongamano
hilo alikufata taratibu za chama hasa ujio wake kwa mujibu wa katiba ya chama
hicho.
“Napenda kuchuka
nafasi hii kwanza kukanusha kuwa kongamano lililofanyika katika kata ya tandale
alikuwa la chama bali ni kongamano walilotumia neno chama kwa lengo la kutimiza
malengo yao binafsi kufatia kukiuka katiba ya chama ambayo inasema kiongozi
yeyote chama wa kitaifa anapotaka kufanya jambo lolote katika ngazi za chini
kumtaarifu katibu wa wilaya husika” alisema Bw Mkandu.



