Rais Museveni Amtumbua Waziri Wa Ulinzi Na IGP
Rais Wa Uganda Yoweri Museveni
Na mashirika ya kimataifa
Generali Kayihura, ambaye ni mkereketwa wa vita vilivyomsaidia rais
Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, kwa wakati mmoja alikisiwa kuwa afisa
mwenye mamlaka makubwa zaidi katika jeshi la Uganda.
Lakini amekabiliwa na shinikizo kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa
usalama.
Zaidi ya wanawake 20 wameuawa katika visa vya mauaji ambavyo
havijatatuliwa katika maeneo yanayouzunguka mji mkuu wa Kampala, na katika
miezi mitatu iliyopita raia watatu wa kigeni pia wameuawa.
Naibu wake Okoth Ochola anashikilia wadhifa huo.
Kwa mujibu wa ujumbe alioandika rais Museveni katika mtandao wa Twitter,
amesema: " Kwa uwezo wa mamlaka niliyopewa kikatiba, nimemteua Jenerali
Elly Tumwiine kama waziri wa usalama. Nimemteua pia bwana Okoth Ochola kama
afisa mkuu wa polisi.
Naibu wake atakuwa ni Brigedia Sabiiti Muzeei.
Mnamo Mei mwaka 2017 Rais Museveni alimteua upya Kayihura kama mkuu wa
polisi kwa muhula mwingine wa miaka mitatu, hadi mwaka 2020.
Uteuzi huo ulikumbwa na mzozo na haukudumu.



