Breaking News

Mhe.Thadey Masawe Amewataka Wananchi Wa Kata Ya Ndugumbi Kutokutupa Taka Ovyo

Diwani Wa  Kata Ya Ndugumbi Mhe. Thadey Masawe Akiongea Na Waandishiwa Habai (Hawapo Pichani) jijini dar es salaam

Na Sala Mlawas
Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini na kupelekea maafa Diwani Wa  kata ya ndugumbi manispaa ya kinondoni jijini dar es salaam mhe. Thadey Masawe amewataka wananchi kutotupa taka ovyo katika mifereji yakusafirisha maji yatokanayo na mvua hizo.

Akizungumza jijini dar es salaam wakati wa ukaguzi na kukabidhi vivuko 21 (madaraja) katika kata hiyo mhe. Masawe alisema vivuko hivyo vitasaidia kutatua kero za wananchi Wa kata hiyo hususani kipindi ambapo watakutwa na maafa yanayoweza kutokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

“Nanatoa wito kwa wananchi wote wa kata hii wajitokeze kwa wingi na washirikiane bega kwa bega vingozi wao katika zoezi la usafishaji Wa mifereji yote sambamba na kutomwaga taka ovyo ili kuondokana na maafa yanayoweza kujitokeza Mara Tu baada ya mvua kubwa kunyesha” alisema Mhe. Masawe.

Pia mhe. Masawe ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa kata ya ndugumbi nawaomba wananchi tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha tunatunza mifereji  hii ya maji kwa kuhakikisha watu hawatupi taka kwani kufanya hivyo tutachangia kupunguza mafuriko ambayo yanasababishwa na mitaro kuziba kutokana na uchafu kujaa kwenye mitaro
Alisema  kwa sasa mafuriko  katika kata yake itakuwa historia Mara baada ya kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa mto ngombe ambao unajengwa na halimashauri ya manispaa ya kinondoni kwa ufadhili wa benki ya dunia.

“Nitoe rai kwa wananchi wanaoishi karibu na mto ngombe kuanzia mwezi wa sita wataanza kulipwa fidia zao ili kupisha kuanza kwa mradi wa upanuzi wa mto huo ili kuondoa kero zinazowakabili wananchi wa kata hiyo” Alisema.
Nae  mwenyekiti wa mtaa  wa makanya kata ya ndugumbi bwana sulemani mwejeka amesema kuwa katika kata yake wananchi wengi wanajitokeza katika swala la usafi kwani MTU yeyote endapo hatatoka hatua zakisheria zitachukuliwa.

Kwa upande wa wananchi wa kata hiyo bw. bwana mgido, kobelo matimba wakizungumzi mradi huo walisema mradi huo utakuwa ni furaja kwao sambamba na kumwomba Diwani huyo kuhakikisha anatatua kero ya ubovu wa madaraja ombi ambalo Diwani huyo amewahakikishia kumaliza changamoto hizo.