Zaidi Ya Kaya 100 Keko Mwanga B Nyumba Zao Kuzingirwa Na Maji.
Zaidi ya kaya 1000 kutoka mtaa wa Keko mwanga B kata ya
Keko hawana mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji
yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari
katika eneo la tukio wananchi hao wamesema tatizo hilo linasababishwa na ujenzi
holela wa miundombinu ya gati ya bandarini ndio chanzo kikubwa kilichopelekea
maji kuingia majumbani mwao na kusababisha kupoteza Mali zao .
Aidha wananchi hao wanaiomba serikali kuweka wakandarasi wenye
uweledi wa hali ya juu kwani iwapo wakandarasi hao wangekua na utaalamu hali
hii isinge adhiri wakazi hao kwani baada ya kuzibua mfereji wa kupeleka
maji baharini badala yake wameziba mianya hiyo yakupeleka maji.
Hata hivyo bwana Leonard manda mmoja
wa wakazi wa mtaa huo amesema kuwa kutokana na mafuriko hayo yaliyotokea hawana
hata maji ya kunywa wa pakulala sababu ambayo imesababishwa na wachina
hao .
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Keko mwanga B bwana
shilingi Hashimu shilingi amesema kuwa wananchi hao waliokumbwa na mafuriko
wameshindwa kuokoa kitu chochote kutokana na ukubwa wa maji yaliyoingia kwani
ni tofauti na miaka mingine.
Bwana Hashimu aliongeza kuwa anatoa
wito kwa serikali isiwatizame watu hao kuwa wamejitakia kwani nyumba hizo
zimejengwa mda mrefu na serikali ilikuwepo ilikua inahitajika waangalie maeneo
yapi Salama na yapi hatarishi wayazuie.
Na Sala Mlawas





