Mtoto Akutwa Na Sindano 7 Za Kushonea Nguo Tumboni

Mtoto wa kike
mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa kijiji cha Keringet kaunti ya Pokot
amekutwa na sindano 7 za kushonea kwa mkono tumboni mwake, baada ya kupigwa
picha ya X ray.
Mtoto huyo
alipelekwa hospitali ya Kapenguria siku ya Jumanne kupata matibabu ya maumivu
ya tumbo ambayo alikuwa akiyapata kwa muda mrefu bila kujua tatizo ni nini.
Bibi yake Bi.
Emily Linga'a ambaye ndiye anayeishi naye, amesema mtoto huyo alikuwa akilalamika
maumivu ya tumbo kwa zaidi ya miaka miwili, lakini hawakuweza kubaini mara moja
chanzo cha maumivu hayo na kuendelea kumpatia dawa za kutuliza maumivu, lakini
baada ya kuona anazidi kualalamika walimpeleka hospitali na kugundua ana tatizo
hilo.
“Kwanza nilidhani
mtoto alikuwa na minyoo, sikuwahi kufikiria kwamba ana sindano tumboni mwake,
nilikuwa nahisi ni malaria siku zote na kumpa dawa za maumivu”, amesema bibi
huyo ambaye anaishi naye, baada ya mama yake kumuacha alipoolewa na mwanaume
mwengine.
Madaktari wa
hospitali hiyo wamempa rufaa ya kwenda hospitali kubwa ya Moi ili kuweza
kufanyiwa upasuaji wa tumbo, na kutolewa sindano hizo ambazo hazijajulikana
zimeingiaje.



