Prof. MBARAWA Azindua Maadhimisho Miaka 50 Ya Bodi Ya Wahandisi Atoa Neno…
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame
Mbarawa (kulia) akibofya rimoti kuzinduwa maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya
usajili ya Wahandisi Tanzania (ERB), kulia ni Mwenyekiti waBodi ya usajili ya
Wahandisi Tanzania, Profesa Ninatubu Lema, Mei 24 katika ukumbi wa karimjee jijini
Dar es Salaam.
Dar
es salaam:
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame
Mbarawa amesema serikali inatambua mchango wa waandisi wazawa na itaendelea
kushirikiana nao katika miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini kuelekea uchumi
wa viwanda.
Akizungumza jijini katika hafla ya uzindua
maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya usajili ya Wahandisi Tanzania (ERB) tangu
kuanzishwa kwake mwaka 1968 alisema katika kipindi hiki cha kujenga uchumi wa
viwanda, bado inakabiliwa na uhaba wa wahandisi wa fani za Bandari, Posta Na
Reli.
“Nia ya serikali ni kuwa na Wahandisi wengi ili kuiwezesha
nchi kufikia ya Viwanda, lakini bado kuna baadhi ya maeneo yana changamoto
ambayo ni uhandisi wa Bandari, Posta, Na Reli,” alisema Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akizungumza kwenye uzinduzi wa
maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya usajili ya Wahandisi Tanzania (ERB) uliofanyika
Mei 24 katika ukumbi wa karimjee jijini Dar es Salaam
Alisema serikali imeandaa mkakati wa kuwashirikisha
vijana kutoka vyuo vikuu wanaosomea fani ya uhandisi katika miradi mikubwa unayofanyika
nchini ili kuwajengea uwezo vijana wa fani kwa manufaa ya baadae.
“Mradi
utakaotekelezwa nchini utakuwa na vijana kutoka vyuo vikuu wa fani ya uhandisi
kwa lengo kutawaongezea ujuzi na uelewa wa wataalamu hao wa uhandisi nchini”
Alisema Prof. Mbarawa.
Aidha
Prof. Mbarawa aliongeza kuwa seriklali ipo katika mpango kabambe wa kuliboresha
shirika la ndege, kutokana na uhaba mkubwa wa wahandisi wa ndege jitihada za
makusudi lazima zichuliwe kwa lengo la kuwaamasisha vijana kusomea masomo hayo
kutaliwezesha taifa kuwa na wahandisi wengi hapo baadaye.
Alisema
zaidi ya Wahandisi 2,000 wanaitimu masomo katika vyuo vikuu nchini kila mwaka,
lakini kati yao ni 800 tu wanaosajiliwa na ERB, hali inayosababisha kuwapo kwa
wahandisi duni nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya usajili ya Wahandisi Tanzania,
Profesa Ninatubu Lema akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya usajili
ya Wahandisi Tanzania (ERB), Mei 24 katika ukumbi wa karimjee jijini Dar es
Salaam.
Mapema akimkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa bodi hiyo,
mhandisi Bw. Ninatubu Lema alisema idadi ya wahandisi waliosajiliwa nchini ni
21, 742 kati ya hao wahandisi wanawake ni 2,153 sawa na aslimia 10.
“Juhudi
zinapaswa kuongezwa katika udahili wa wanafunzi katika vyuo vikuu, kwa maana idadi
ya wanafunzi wa kihandisi wanaodahiliwa katika vyuo vikuu inapungua kila
mwaka,” alisema Lema.
Aidha Mhandisi Lema amezitaja changamoto inayoikabili taaluma ya uhandisi ni
uhaba wa wahandisi, uhaba wa bajeti, uhaba wa rasiliamali watu na fedha na
hivyo kama kozi za uhandisi zitaongezwa Katika vyuo zitaleta tija baadaye.



