Rais MAGUFULI Anusa Ufisadi Wa Bilioni 8 Ukumbi Wa Chuo Cha Mkwawa....Atoa Maagizo Mazito Kwa Vyombo Vya Dola

Rais John Magufuli amefichua siri ya kukataa
kuweka jiwe la msingi katika ukumbi wa jengo lililopo katika Chuo Kikuu
Kishiriki cha Mkwawa mkoani Iringa akisema limejengwa kifisadi kwa Sh 8bilioni.
Rais ameeleza hayo jana, Mei 2, 2018
wakati akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho ikiwa ni sehemu ya
ziara yake mkoani humo.
"Muda mwingine tuambizane ukweli
Chuo cha Mkwawa kimeniangusha, ndio maana nilikataa kuja kuweka jiwe la msingi
katika lile jengo. Siwezi kuweka jiwe la msingi katika jengo la kifisadi.
"Nikitoka hapa nitakwenda
kulikagua. Nilitegemea chuo hiki kitasimamia value of money (thamani ya fedha),
kwa sababu kuna wasomi lakini tofauti."
Rais Magufuli alitumia nafasi hiyo
kuviagiza vyombo vya dola kuhakikisha wanawachukulia hatua wale wote
waliohusika katika mchakato huo hata kama wamestaafu, watafutwe waliko.
"Mmeshindwa kusimamia ujenzi wa
lile jengo halafu leo mnaniomba mabweni? Nitaanzaje kuwakubalia wakati huku mmeshindwa,
siwezi. Vyombo vya dola na wizara vifuatilie mkishindwa nitafuatilia.



