Breaking News

Tamasha la Kumbukizi Vita vya Maji Maji na Tamasha la Utalii wa Utamaduni kufanyika Feb 22-27 Miji Songea

Wizara ya maliasili na Utalii kupitia  Taasisi ya Makumbusho ya Taifa, imeandaa tamasha la kumbukizi ya vita vya maji maji sambamba na tamasha la utamaduni litakalofanyika terehw 22 hadi 27 February mjini Songea.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Biseko Lwoga alisema lengo kubwa la kuandaa tamasha hilo ni kutoa fursa watanzania kujifunza historia ya vita hiyo sambamba na kuenzi, kutunza na kuendeleza urithi asili.

"Lengo kuu la tamasha hili ni kutoa fursa kwa watanzania kujifunza juu ya histori ya vita ya majimaji pamoja pamoja na tamasha la utamaduni ni kuenzi, kutunza na kuendeleza urithi asilia" Alisema Dkt. Lwoga.

Alisema kumbukizi hii ni kuwakumbuka na kuwaenzi babu zetu waliokufa wakitetea maslai ya nchi yetu.