BREAKING NEWS: ZITTO, Maalim SEIF Washinda Kwa Kishindo

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Taifa wamemchagua Mwami Ruyagwa Kabwe Zitto Zuberi kuwa KIONGOZI WA CHAMA kwa kura. 276 sawa na asilimia 73.6%.
bwana Ismail Jussa Ladhu aliekuwa mshimdami wake amepata kura 91 sawa na asilimia 24.2% wakati Kura 8 za wajumbe zimekataliwa (kuharibika).

Katika hatua nyingine wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Taifa wamemchagua Maalim Seif Sharif Hamad kuwa mwenyekiti wa Chama Taifa kwa kura 337 sawa na asilimia 93.35%
Waliokuwa mshindani wake katika nafasi hiyo bwana Yeremia kulwa Maganja amepata kura 20 sawa na asilimia 5.55%, huku bwana Shilungushela Nyangaki akipata kura 4 sawa na asilimia 1.10%, ambapo kura za wajumbe 2 zimekataliwa (kuharibika).
Uchaguzi huo ambao umefanyika 14 march 2020, katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es salaam. ulisimamiwa na Mwenyekiti wa KAMATI Maalumu ya Uchaguzi Taifa Msomi Wakili Ndugu Omar Said Shaban.



