Dkt MJEMA Mgeni Rasmi Siku ya Wanawake Tabata

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dkt. Sophia Mjema anatajia kuwa mgeni ni rasmi siku ya Kongamano la Umoja wa Wanawake Kata ya Tabata UWT itakayofanyika Ijumaa Machi 27 ukumbi wa Latino Inn.
Madhimisho ya kongamano lilo litaongozwa na Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema na Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus kuanzia saa mbili asubuhi ambapo siku hiyo kutakuwa na maonyesho ya wanawake wajasiriamali yatakayotangulia na shughuli za kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa Kongamano hilo Mjumbe wa Halmashauri kuu Tabata MTAMBAN Heri Shaaban alisema maandalizi yote yamekamilika kufanikisha siku hiyo kwa kushirikiana na UWT Tabata.
Heri alisema wengine watakaopamba siku hiyo Warembo wa Miss Ilala na madiwani Wanawake wa halmashauri ya manispaa ya Ilala.
"Kongamano la kwanza la siku ya Wanawake Tabata limeandaliwa na mimi kwa kutambua mchango wa wanawake na vijana wilayani Ilala, Octoba 05/2019 nilitununikiwa tuzo na mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete tuzo ya Ubunifu ya maswala ya Wanawake na vijana iliyotolewa na Utalii 255 Tanzania ambapo Mwenyekiti wake Mbunge Angelina Malembeka tuzo hii ndio imenipa hamasa kuwaanda jambo hili kwa siku hii muhimu kufurahi na wanawake wa Tabata hususani kata ya Tabata " alisema Heri.
Aidha alisema siku hii muhimu kwa Wanawake wa Tabata kuelezea changamoto zao sambamba pia watapata elimu ya malezi kwa vijana kuhusiana na elimu ya Afya ya uzazi kutoka kwa wataalamu ofisi ya Mganga Mkuu pamoja na elimu ya ujasiriamali na mikopo kutoka kwa Afisa maendeleo Manisipaa ya Ilala.
Aidha Mratibu Heri Shaaban alisema Kata ya Tabata hilo ni kongamano la kwanza la siku ya Wanawake ambapo litakuwa endelevu kila mwezi March



