NCCR Mageuzi Yatoa Ufafanuzi Juu Waraka Uliosambaa Katika Mitandao ya Kijamii
Chama cha NCCR Mageuzi kimewataka watanzania kupuuza waraka unaodaiwa kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho kwenda kwa wajumbe halmashauri kuu
ambazo umekuwa ukisambazwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari nchini hususani .
Akizungumza jijini Dar es salaam Makamu Mwenyekiti bara Anjelina Mutahiwa alisema waraka huo ambao umetolewa tarehe 12/ 03/ 2020 kwa lengo kuwa na nia ovu ya kuchafua utu pamoja na kuaribu taswila ya chama kwa jamii.
"Nitoe wito kwa watanzania kuuza waraka ambao unasambaa katika mitandao ya kijaamii na baadhi ya magazeti wa uzushi, uzindaki na uchochezi na wenye nia ovu ya kukichafua chama" Alisema Bi Mutahiwa.
Alisema chama tayali kimeshachukua hatua kwa kutoa malalamiko kwa mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA na nakala kumpatia msajili wa vyama vya siasa nchini kukanusha juu ya waraka huo na kumwomba kufanya uchunguzi wa kina wakibainika wahusika wachukuliwe hatua.
Katika hatua nyingine Bi,Mutahiwa amezungumzia mwenendo wa ugonjwa wa homa ya mapafu COVID-19 nchini amesisitiza wananchi kuendelea kutumia ushauri ambao unatolewa na wataalam wa afya hili kuweza kujinga na janga hilo.
Alisema chama chake kitaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kinatoa elimu kwa wananchi pamoja na kitoa ushauri kwa serikali juu yaa hatua mbalimbali za luchikua kujikinga na ugonjwa huo kama alivyofanya mwenyekiti wake ambae ni mtaalam wa kupambana na majanga mapema 17 machi mwaka huu.
Aidha makamu mwenyekiti huyo ametoa wito kwa watanzania wote kushikamana kwa kufata maelezo sahihi ya wataalam pamoja na kuitaka serikali kuwekeza zaidi kwa kulinda afya za wananchi.




