DC Jokate Mmwegelo Atimiza Ahadi Kwa Akina Mama KISARAWE
Aidha, aliwapongeza wadau kwa kumuunga mkono mpaka kufanikisha ujenzi huo ambao anaamini utakuwa chachu kwa akina mama hao.
"Niwashukuru Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa mchango wao na Halmashauri ya Wilaya Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa usimamizi mzuri mpaka sasa.
Lakini pia kampuni ya Coca-Cola. Kuna mambo mazuri tutafanya zaidi hapa kijiji cha Masaki" Alisema Jokate.
DC Jokate pia alimshukuru, Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kupeleka maendeleo kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
"Baada ya Mhe Rais kufanya ziara Kisarawe na kuelekeza barabara kukarabatiwa kwa kiwango cha lami kutoka Kisarawe mpaka Vikumburu kuelekea Hifadhi mpya ya Taifa ya Mwalimu Nyerere.
Sisi viongozi hatujalaza damu. Tumeanza kutengeneza fursa kwa wananchi hasa za maeneo ya Watalii ikiwa ni pamoja na kupata chakula cha Asili na jengo ili la kisasa ni kielelezo" Alimalizia Jokate.
Muonekano wa jengo hilo la kisasa ambalo limekamilika kwa asilimia 90.






