Katibu Mkuu wa ALAT Aridhishwa Ubunifu na Kasi ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Miradi Manispaa Ilala.. Atoa Neno Kwa Halmashauri Zingine Nchini


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Elirehema Kaaya amezitaka Halmashauri nchini kuiga mfano kwa Manispaa Ilala kwa kuwa wabunifu katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo hususani ujenzi.
Akizungumza mara baada ya ziara ya kujionea na kukagua miradi ambayo inatekelezwa na Manispaa ya Ilala alisema utaratibu huo wa kujenga majengo ya gorofa hususani katika maeneo yaliyo na uhaba wa ardhi hasa
"Nitoe rai kwa manispaa zingine na majiji kuiga mfano wa manispaa ya Ilala kwa kujenga majengo ya gorofa kutokana na changamoto ya ufinyu wa maeneo mijini"
Alisema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe magufuli imekuwa mstali wa mbele katika kuhakikisha inatenga fedha katika kutekeleza miradi ya Afya, elimu na miundombinu kwa lengo ya kumaliza changamoto hivyo kuzitaka manispaa zote kuzitumia fedha hizo kwa kama ilivyopangwa.
Aidha bw. Kaaya ameipongeza manispaa ya Ilala kwa kusimamia na kuratibu miradi hiyo kwa viwango vya hali ya juu hivyo kuridhishwa na utekelezaji wa miradi.
Miradi aliyoitembelea ni Kituo cha Afya Buguruni, Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya sekondari ya Ilala Kasulu na Zahanati ya Kipawa.





