Mchugaji Kagia: Wasabato Tuiombee Nchi Kuelekea Uchaguzi Mkuu
Waumini wa dhehebu la Wadventista Wasabato nchini wametakiwa kuendelea kuliombea taifa kuelekea uchaguzi mkuu hili uwe wa amani na utulivu utakaofanyika 28 Oktoba 2020.
Akizungumza katika ibada ya kufunga makambi jijini Dar es salaam mchungaji kiongozi wa kanisa Advestista Mtaa wa Ilala, Israel Kagia alisema leonga la ibada hii kufanya maombi kuombea amani na kushukuru kwa mapito yote kama taifa.
"katika kipindi cha juma zima tumekuwa tukifanya maombi, kumuomba mwenyezi Mungu kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano hasa kuelekea katika uchaguzi mkuu wa Urais, wabunge na madiwani" Alisema mchungaji Kagia.
Alisema katika kipindi hicho cha siku saba za makambi kanisa lilishirikiana na makanisa mengine ya wasabato ya Ilala, Buguruni, na Kigogo.
Katika hatua nyingine Mchungaji Kagia amempongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa juhudi na hatua za dhati alizochukua katika kupambana na Ugonjwa wa Covid-19.
Mapema akizungumza katika ibada hiyo mchungaji mwakilishi kutoka Arusha , Baraka Laizer alisema ibada kama hii ya makambi hufanyika mara moja kila mwaka kwa lengo la kufundisha mambo ya kiroho kwa wahumini.
Alisema katika kipindi chote cha siku saba za maombi waumini walifundishwa na kupatiwa elimu afya pamoja na mafundisho ya ndoa kutokana ndoa nyingi kuwa na changamoto ya kuvunjika kutokana na wanandoa kutofuata misingi ya Biblia.
Naye Mchungaji Sadeck Rugumyamiheto alisema ibada hii ya makambi walijadili maswala mbalimbali ikiwemo changamoto ya vijana kutofunga ndoa.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam




