Profesa LIPUMBA: Awatoa Hofu WanaCUF na Wananchi kuhusu Pingamizi
CHAMA Cha wananchi CUF kimemtaka Mgombea urais wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu kuja na hoja za msingi za kidemokrasia zitakazo lisaidia Taifa na si kuleta taharuki kwa wananchi.
Akitoa ufafanuzi huo makao makuu ya chama hichi jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amewataka wananchi na wanachama wa chama hicho ambao walipatwa na taharuki baada ya kuona taarifa hiyo katika Mitandao ya kijamii kuwekewa pingamizi.
"Kuna hoja nzito za kuzungumza kwenye jamii kuelekea uchaguzi mkuu na si kuleta hoja za kuleta pingamizi ambazo hazina mashiko kwa Taifa na mbaya zaidi nimeshangazwa na uanasheria wa Lissu kwa hoja ya pingamizi alilotoa.kwamba chama kimefuata maelekezo ya tume ya uchaguzi na siyo kanuni na sheria za uchaguzi." alisema Prof. Lipumba
Alisema Taifa linaingia katika uchaguzi lakini wameona kuna Mambo mazito yanaendelea na Lissu ni mwanasheria lakini aneshindwa kutumia sheria kujenga hoja zenye kuleta Demokrasia ila wanataka kuingia madarakani tu bila kufuata sheria na kanuni za uchaguzi.
Aidha Prof Lipumba aliongeza kuwa anamshangaa Lissu pamoja na kuwa mwanasheria mbobezi lakini anatoa hoja dhaifu kuhusu pingamizi na kuwataka wana chadema wamsaidie kwani inawezekana anaomba huruma ya wananchi ili wamchague kutokana na changamoto aliyokutana nayo.
Lipumba alihoji kwamba mbona mgombea wa Act-wazalendo Bernard Membe ambaye amerudisha fomu kwa sheria hizi hizi hawajamuwekea pingamizi, wanajua kwamba Lipumba ni mtu wa mpingo na ana hoja za msingi kuelekea uchaguzi mkuu.
"Leo CHADEMA na Lisu wanazuia Uhuru wa wananchi wa kupiga kura kwa mgombea wanaye mtaka kwa kuweka pingamizi ambalo halina mashiko lakini niwatoe hofu wanachama na watanzania kwamba Cuf imejipanga na tunakwenda kwenye kupeleka Sera nzito kwa ajili kuleta furaha kwa watanzania." Alisema Profesa Lipumba.
Lipumba kutokana na kupata taarifa za pingamizi hilo wao Kama chama wameshaweka kila kitu sawa na wamewaondoa hofu watanzania nakwamba watashiriki uchaguzi Kama kawaida na mapema watatangaza kuaza kwa kampeini.
Kwaupande wake mwanasheria wa chama hicho salvatory Magafu Alisema changamoto iliyojitokeza kwa Lissu nikwasababu kabla ya kufikia mchakato wa kuchukua na kurudisha tume ya uchaguzi ulikutana na vyama vya siasa na wakashauliana na kukubaliana Mambo mbalimbali na kwa bahati mbaya Lissu alikuwa nje ya nchi.
"Ndugu zangu waandishi hapa tatizo nikwamba lissu hakuwepo nchini na alipofika amefikia kugombea tu urais na nashangaa hata chama chake kupitia mwenyekiti wake Freeman Mbowe hawana ukaribu na Mgombea wao kwani wangekuwa karibu naye
wangemshauli." Alisema Magafu.
Magafu aliongeza kuwa Tundu alikuwa mwanasheria zamani lakini sasahivi amekuwa na changamoto hivyo wanachama na wananchi wasiwe na hofu yoyote.




