Profesa Lipumba Azindua Mpango wa Kuchangia CUF kuelekea Uchaguzi Mkuu
Mwenyekiti wa Chama cha wanachi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba amezindua mpango kukichangia chama hicho ambapo wanachama na wananchi wenye mapenzi mema wataweza kukichangia kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema lengo la kuzingua mpango huo ni kukiwezesha chama cha wananchi kuweza kushiriki kikamilifu na kuweza kufikia dhamira ya chama kushika dola.
"Sababu ya kuanzisjwa kwa mpango huu ni kuwezesha chama kuweza kujiendesha katika kipindi chote cha kampeni badala ya kutegemea ruzuku ambayo aiwezi kutosha"
Alisema mtu mwenye akili timamu awezi kwenda katika uchaguzi mkuu kwa kutemea ruzuku kwani ni sawa na kuandaa anguko lako mwenyewe.
Profesa lipumba amewataka wananchi na wapenzi wema wa chama hicho kujitokeza kuchangia hili kuweza kufanya vizuri katika uchaguzi kwa kuchangia kupita Akanti ya Benki ya NMB tawi la temeke akaunti namba 20710050166.
Amezitaja kwa wanaotumia mtandao wa simu za mkononi ni M.Pesa namba 0762469342, Tigo Pesa 0658111925 na kwa naetumia mtandao wa airtel ni 06699533883.




