Breaking News

Rose Muhando, Bonny Mwaitege kupamba Tamasha la Kuombea Taifa Kuelekea Uchaguzi Mkuu 23 Agost Jijini Dar

Maandalizi ya Tamasha kubwa la kuombea uchaguzi mkuu 2020 ambalo limeratibiwa Kampuni ya Msama Promotion limeendelea kupamba moto kufatia orodha ya waimbaji wa nyimbo za Injili kuongezeka akiwemo Mchungaji Faustin Munishi pamoja na Jacob Chengula.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama alisema maandalizi ya tamasha hilo ambalo linatarijiwa kufanyika Agost 23 jijini Dar es salaam yanaendelea vizuri katika nyanza zote kufaitia kuongezea waimbaji zaidi watakao tumbuiza siku hiyo

Aliwataja Waimbaji wengine ambao wataimba siku hiyo kuwa ni pamoja na Christina Shusho, Christopher Mwangira pamoja na kwaya mbalimbali ambao tayali wapo kambini wakiendelea na mazoezi ili kuhakikisha wanafanya vizuri siku ya tamasha.

“Tumejiandaa na utaratibu wote unakwenda vizuri ikwemo usalama wa kila mshiriki kwani Jeshi la Polisi Kanda maalum wamejipanga kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika ulinzi” Alisema Bw. Msama.

Alisema tamasha hilo ambalo litaanza kuanzia saa 6 mchana na kuendelea hivyo kuwataka wakazo wa jiji la Dar es salaam na mikoa jirani bila kujali dini wala itikadi zao kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwan tamasha hilo ambapo halitakuwa na kiingilio.

“Waimbaji wote wa nyimbo za Injili tayali wapo kambini wakiendelea na mazoezi katika kuhakikisha wanashiriki vyema kuombea uchanguzi mkuu ufanyike kwa amani na utulivu” Alisema Bw. Msama.

Bw. Msama aliongeza kuwa pia katika tamasha hilo amewaalika maaskofu kutoka madhehebu tofauti, viongozi wa serikali na taasisi binafsi ambao watashiriki katikaa tamasha hilo kwa ajili ya kuliombea taifa kuelekea uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu.

“Nchi Tumepita katika mapito mbalimbali ikiwemo janga la Ugonjwa wa COVID-19 watanzania tujitokeze tuungane pamoja katika kuliombea taifa ili uchaguzi mkuu ufanyike kwa amani na utulivu” Alisema Bw. Msama.