Waziri wa Kigwangala Azindua Muhuri wa Usalama Kutoka Baraza la WTTC
Waziri wa
Maliasili na Utalii Khamisi Kigwangala amezindua rasmi Muhuri wa usalama
kutoka Baraza la usafiri na Utalii dunia WTTC uliopokelewa nchini Julai 22
mwaka huu.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa Muhuri huo jijini Dar es salaam, Waziri Kigwangala
ameushukuru uongozi wa awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kwa umahiri
ulionekana kwa kuthibiti ugojnwa wa Covid 19, na kupelekea Tanzania kufungua
mipaka huku tukichukua hatua madhubuti katika kujinga na ndio sababu kubwa
inatufanya leo kuwa hapa na kutumia muhuri wa usalama.
Aidha Kingwangala
amempongeza katibu mkuu mpya wa wizara ya maliasili na utalii Aloyce Nziku kwa
juhudi walizozifanya katika kipndi chote cha Covid 19, kwa kutokusita
kushirikiana na balozi za Tanzania kuifikia dunia na kutangaza utalii wa Nchi.





