LHRC Kuwakutanisha Wadau wa Haki za Binadamu Katika Kongamano Kubwa, Kilele cha Maadhisho ya Miaka 25 Tangu Kuanzishwa Kwake Jijini Dar
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu Bi. Anna Henga alisema katika maadhimisho hayo kutafanyika shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na kufanya tathimini ya haki za binadamu nchini.
"Katika kilele cha siku cha maadhimisho tumeandaa shughuli mbalimbali za kijaamii pamoja na kupata wasaa wa kukutana na wadau wetu kutizama tulipotoka, kufanya tathimini ya hali tulionayo kuweka mikakati ya mbeleni" Alisema Bi Henga.
Alisema pia kutakiwepo na mijada ya hali ya haki za binadamu nchini tangu kuanzishwa kwake nchini, sambamba na mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya sheria na haki za binadamu.
Maadhimisho ya mwaka huu ambayo yatafanyika katika ukumbi wa Julias Kambarage Nyerere Hall na kuwakutanisha Viongozi wa Serikali, Watetezi wa haki za binadamu, Vingozi wa Dini, Wanasisa, Wanafunzi na Wanazuoni.
Maadhimisho ya mwaka huu yamepewa Kauli mbiu "Haki ni Maendeleo, Simamia Haki"




