NEC: Tunaongozwa na Sheria si Kwa Mashinikizo.. Toa Sera Matusi, Kashfa Avitavumilika
MKURUGENZI wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mehera Charles amevionya vyama vinavyotoa matusi kwenye kampeni zao vitachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na vyama hivyo kufungiwa kufanya kampeni.
"Sisi kama NEC tukiona kama kuna chama kinatoa matusi kwenye kampeni badala ya kunadi sera tutakifungia chama hicho kufanya kampeni hata kama kitaenda Ulaya kulazimika tutakifungia," alisema
Akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja kwa watoa huduma za habari mitandaoni jijini Dar es salaam Bw. mahera alisema kukuwepo na baadhi ya vyama siasa ambavyo vimekuwa vikitoa lugha za matusi na za uzalilishaji jambo ambalo ni kinyume na maadili ya uchaguzi.
"Hata kama kipindi hiki ni cha kampeni, lakini ifahamike kuwa sheria nyingine zote zinaendelea kufanya kazi hivyo hatutasita kuchukua hatua stahiki pale ambapo itabidi kufanya hivyo"
Aidha, amewapongeza watoa huduma mitandaoni kwa kutoa taarifa za uchaguzi na kwamba watoa huduma mitandaoni ni wadau muhimu wa uchaguzi na kuwataka kuhakikisha utoaji taarifa unakuwa uendelevu kudumisha amani.
Bw. Mahera amevitaka vyombo hivyo kuendelea kuhamasisha watanzania ili wajitokeze siku ya uchaguzi kwa ajili ya kupiga kura na kwamba ushirikiano na vyombo hivyo utafanikisha mchakato mzima wa uchaguzi.
"NEC inapenda kutoa rai kwa vyombo vya habari mtandaoni kutoa taarifa sahihi na kwa wakati na kutotoa taarifa bila upendeleo wa kuangalia vyama na badala yake watende haki kwa wagombea wa vyama vyote"
Alisema NEC haitafanya kazi na majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi na sio kwa mashinikizo ya matafaifa ya nje na kuitaka vyama hivyo kuzingatia sheria.




