RC KUNENGE: Wanawake Jitokezeni Kwa Wingi Kuchangamkia Fursa
Mkuu Wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa wito Kwa wanawake nchini kujiamini na kuonyesha uwezo wao kwenye nafasi mbalimbali wanazopatiwa ili waweze kufanikiwa katika kila jambo.
Akizungumza katika ufunguzi Wa Mkutano uliowakutanisha Viongozi Wa Dini, Wanasiasa na Watetezi wa haki za wanawake uliolenga kuhamasisha amani, Umoja na Haki alisema anaamini wanawake wanao uwezo Mkubwa wa kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii hivyo amewataka kutumia vizuri nafasi zao.
Aidha RC Kunenge alisema serikali ya Mkoa Wa Dar es salaam itaendelea kulinda na kuweka mazingira mazuri ya kuhakikisha haki ya kila mmoja inalindwa na kuheshimiwa Kwa mujibu Wa sheria.
"Natoa wito Kwa wananchi kulinda amani, utulivu na upendo Kwa mustakabali Wa maendeleo na kuwakumbusha kuhudhuria mikutano ya kampeni ili waweze kupima sera za wagombea" Alisema RC Kunenge
Mkutano huo wa kuhamasisha amani na haki umeandaliwa na chama cha wanahabari Wanawake Tanzania TAMWA Kwa kushirikiana na taasisi ya Amani Tanzania ambapo tayari mikutano ya aina hiyo imeshafanyika kwenye kanda za Arusha, Dar es salaam, Dodoma na Zanzibar.





