MUSIBA: Na Taarifa za Uwepo wa Vikundi Vya Vijana Vinavyoratibiwa Kufanya Vurugu Siku ya Uchaguzi, Awaasa Vijana Kujitenga na Mpango huo wa Kuvuluga Amani
Watanzania wametakiwa kuwa makini na kulinda Amani, Umoja na Mshikamano kuelekea uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020 kufatia kuwepo kwa viashiria vya baadhi ya vikundi vyenye nia ya kutaka kuleta vurugu.
Taadhari hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam Mwanaharakati huru bw. Cyprian Musiba wakati akizungumza na waandishi wa habari kufatia kupata taarifa za uwepo wa vikundi vya vijana ambavyo vinatlratibiwa na baadhi ya vyama vya siasa kwa lengo la kufanya vurugu siku ya uchaguzi.
Alisema Amani, Umoja, mshikamano na upendo uliopo Tanzania tunu ambayo imekuwa nguzo kubwa hivyo itakiwa kulindwa na kutunzwa na kila mtanzania kwani ndio nguzo kubwa ya maendeleo na uendeshaji wa miradi mikubwa yenye tija kwa Taifa.
“Kuna kundi la WhatsApp ambalo lina wafuansi nchi nzima kwa ajili ya kumwaga damu, sijui kwa nini wanataka kuondoa amani iliyopo wanataka kuipeleka nchi kwenye machafuko”alisema Musiba.
Alisema kundi hilo la vijana ambao wengi wao wanasidikika kuingia nchini kutokea nchi jirani za Tanzania wamingizwa nchini na kusambazwa nchi nzima kwa ajili kufanya vurugu siki uchaguzi mkuu endapo mgombea wa chama chao hatotangazwa hivyo ametoa tahadhari kwa wazazi na vijana kujiepusha na vurugu hizo.
Aidha bw. Musiba alionheza kuwa, vijana hao pia wamekiwa wakipanga mbinu chafu mbalimbali ikowemo kuwalaghai wananchi kwamba watawawezesha kupata mikopo.
"Binafsi kama mwanaharakati huru kazi yangu kubwa ni kutoa taadhali wala sina nia mbaya wananchi kwa Tanzania bali ni kuondoa taharuki kwa wananchi, kufatia mpango huo wa kuleta vurugu na hatimae nchi kuingia kwenye machafuko".
Akizungumzia mafanikio ambayo yamepatikana kipindi cha uongozi wa awamu ya tano Tanzania imefanikiwa kuwa na miradi mikubwa iliyotatua changamoto za wananchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya madaraja, reli na uzalishaji wa umeme Rufiji.
" Hivyo napenda kuvhukua fursa hii kuwaasa wazazi na walezi kuwa makini na vijana wao kwani mpango huu ni moja ya mbinu ambayo imekuwa ikitumiwa na mataifa ya magharibi kwa nchi za kiafrika ambazo zimebarikiwa uwepo kwa asilimali kubwa za hasa madini ukiangalia mfano LIBYA na DRC"




