Breaking News

WAMBURA: TUNAIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO

Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Madini wadogowadogo John Wambura ameiomba serikali kuwawezesha wachimbaji wadogo kwenye upatikanaji wa mitaji na elimu ya madini kwani wao ndio wagunduzi wa kubwa wa maeneo yenye madini.

Hayo ameyasema leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini ambao umefungwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Rais Wambura amesema kuwa uchimbaji madini unalipa na unafaida hivyo vijana wawekezaji katika sekta hiyo na kuachana na fikra potofu za kuamini kuwa biashara ya madini ni mpaka ufanye kafara.

Aidha ameongeza kuwa ajira nyingi zinapatikana katika sekta ya madini hivyo wachimbaji wafuate sheria ya uchimbaji madini pamoja na kuwahamasisha vijana kuchangamkia frusa hizo.

Hatahivyo ametoa wito kwa makampuni makubwa ya uchimbaji katika kurudisha kwa jamii kile wanachopata wasiishie tu kuwajengea shule hospitali na maji tu bali wawapatie na elimu kuhusu madini.

Sambamba na hayo amesema kmkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini umekuwa na matokeo chanya hivyo amewasisitiza wanachama wa shirikisho hilo kujitojeza kwa wingi katika mkutano ujao.