KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA KIWANDA CHA VIUADUDU WA MALARIA TANZANIA BIOTECH PRODUCTION LIMITED KIBAHA
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Daniel Sillo ambaye pia ni Mbunge wa Babati Vijijini akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutembelea kiwanda cha viuadudu wa malaria cha TANZANIA BIOTECH PRODUCTION LIMITED kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe akielezea namna serikali ilivyojipanga na kuweka mazingira wenzeshi baada ya kumaliza kutembelea kiwanda cha viuadudu wa malaria cha TANZANIA BIOTECH PRODUCTION LIMITED kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo Tanzania (NDC), Dkt. Nicholaus Shombe akielezea malengo ya ziara hiyo mara baada ya kumaliza kutembelea kiwanda cha viuadudu wa malaria cha TANZANIA BIOTECH PRODUCTION LIMITED kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Kibaha:
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Bajeti imetembelea kiwanda cha viua dudu wa Maralia (Tanzania Biotech Products Limited) kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Daniel Sillo ambaye pia ni Mbunge wa Babati Vijijini amesema wamefika kiwanda hapo kiwa ni mwendelezo wa ziara yao ya siku mbili ambayo walianzia mkoani Dar es Salaam.
“Tumefanya ziara ya kutembelea kiwanda hiki kujiona hali ya uzalishaji wa dawa hii ya kuua viluilui vya Mbu, lakini pia kuona kama kuna changamoto za kibajeti pia,” Alisema Mhe Sillo.
Mhe Sillo ameeleza kuwa kiwanda hicho kitafanya uzalishaji vizuri hakutakuwa na haja ya kuagiza vyandarua kutoka nje ya nchi kwani itataosheleza kuua viluilui vya Mbu na hivyo kuepukana na ugonjwa wa Malaria.
Alisema kiwanda hicho ni muhimu sana kwani kitasaidia kuimarisha afya za wananchi na kuongeza uzalishaji kwa manufaa ya ukuaji wa uchumi wa nchi kufatia kazi nzuri inayofanywa ya uzalishaji.
Nae Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe ameelezea kamati hiyo namna ambavyo kiwanda hicho kinazalisha viua dudu ambavyo vinatumika kuua viluilui vya mazalia ya Mbu.
“kumekuwepo na changamoto kubwa sana kwa Mbu wanaoeneza Malaria Tanzania na tunatumia fedha nyingi kwa ajili ya kutibu ugonjwa huu,” amesema Kigahe.
Alisema Serikali imekuwa na nia ya dhati kwa kuchukua hatua mbalimbali sambamba na kuhakikisha mazalia ya Mbu yanaangamizwa.
“Nazani mmeona jinsi kiwanda hiki kinavyofanya kazi lakini bado zipo changamoto ambazo tunaamini baada ya kamati hii kujionea itaweza kutoa mkazo zaidi kwa Serikali kuendelea kutenga bajeti ya kutosha ili tuzalishe zaidi,” alisema Kigahe.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo Tanzania (NDC), Dkt. Nicholaus Shombe alisema kiwanda hicho moja ya viwanda vilivyopo nchini vya kipekee.
“Kiwanda hiki cha kipekee ambacho kinauwezo wa kuzalisha bidhaa karibu Sita, tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa kinazalisha viuadudu tu vya Mbu,” amesema Dkt. Shombe.
Ameeleza kuwa kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha bidhaa kama dawa ya kuulia wadudu kwenye mimea, mbolea ambayo haina kemikali.



