SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BANDARI
Na Timoth Marko
Serikali imesema itaendelea kuboreshaa miundombinu ya reli ya mwendokasi (SGR) katika bandari ya Dar es Salaam (TPA) ili kuboresha usafirishaji mizigo kutoka bandari kuwa na ufanusi zaidi.
Akizungumza katika ziara ya kamati ya bunge miundombinu na uchukuzi mkurugenzi wa mamlaka ya bandari (TPA), Bw. Eric Hamis amesema kamati hiyo imetoa mapendekezo ya uharakishaji wa mizigo kutoka bandari ili kuweza kuchochea shughuli za kiuchumi.
"Tnaendelea kuzungumza na tanesco ili wafunge Substation ambayo itasaidia kuharakisha ufanisi wa SGR" Alisema Bw. Hamis.
Alisema mchakacho wa maboresho ya miundombinu ya reli ambao mradi huo unatarajiwa kukamilika mwaka huu.
"Awamu ya pili ya ukamilishwaji wa maboresho ya bandari utakao malizika mwaka 2024 itaenda sambamba na ujenzi wa ghati" Aliomgeza bw. Hamis.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya bunge ya miundombinu na usafirishaji, mhe Japhet Asunga alisema serikali tayali imewekeza zaidi ya dola mil 21 kwa ajili ya ukarabati na upqnuzi wa bandari.
Alisema lazima shirika hilo la bandari kuangalia riba unapo agiza mizigo hili kuongeza na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia badari.
"Ni lazima bandari kufanya maboresho kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na biashara nchini na nchi za jirani ili kuwavutia watumie bandari yetu" Alisema mhe. Asunga



