Breaking News

WAWEKEZAJI 24 KUTOKA NCHINI QATAR WATEMBELEA TIC

Kituo Cha Uwekezaji Nchini (TIC) kimepokea wawekezaji 24 kutoka Nchini Qatar ambao wamekuja kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Akizungumza Mara baada ya kuwasili wawekezaji hao Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bi. Anna Lyimo  amesema ujio wa wawekezaji hao ni kufatia ziara ya Viongozi wa TIC nchini Qatar ambapo walikutana na kufanya mazungumzo na Wafanyabiashara kutoka shirikisho la Wafanyabiashara la Qatar KERALA BUSINESS FORUM.

"Leo tumepokea wafanyabiashara 25 ambao wamekuja kuangalia fursa za kuwekeza Kati sekta mbalimbali ikiwemo Mifugo, Vifaa tiba, Utalii, Madawa, sekta ya anga pamoja na masuala ya uchumi wa Bluu" Alisema Bi. Lyimo. 

Alisema kufatia uwepo na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini pamoja na kukuwa kwa diplomasia nchini imekuwa chanzo cha wawekezaji wengi hivyo kuwasihi wawekezaji toka ya ndani wajiunge na TIC kuweza kupata taarifa mbalimbali za fursa ya Uwekezaji Nchini.

Amendelea kusema kuwa wawekezaji hao wanatarajiwa Machi 29 kutembelea Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuangalia fursa ya Uwekezaji lakini kwa Sasa TIC inawapitisha katika taratibu mbalimbali za Uwekezaji pamoja na masuala ya vibali vya kuwekeza Nchini.

Mapema Raisi wa Shirikisho la wafanyabiashara Nchini Qatar Bw.Shanavas Bava amesema wamekuja kuangalia fursa zakuwekeza hapa Nchini kutokana na Tanzania kuwa na fursa nyingi lakini pia kuwepo na mazingira mazuri ya kiuwekezaji ni jambo lililowavutia kuja kuwekeza.

"Tumekuja kuangalia fursa zilizopo za uwekezaji kufatia kuridhishwa na uwepo wa mazingira mazuri ya uwekeza nchini" Alisema bw. Bava