JAKAYA KIKWETE FOUNDATION KUCHANGISHA FEDHA KUBORESHA KITENGO CHA UZAZI SALAMA
Hospitali ya CCBRT kupitia kitengo chake kipya cha afya ya uzazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete wameandaa chakula cha usiku cha hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha zitakazotumika kutoa huduma ya uzazi salama kwenye kitengo hicho.
Kitengo hicho kitatua changamoto zinazowakabili akina mama wajawazito walioko katika mazingira magumu na uzazi hatarishi Wanawake wajawazito wenye ulemavu, wenye historia ya fistula na mabinti wanaopata ujauzito wakiwa na umri mdogo.
Alisema hospitali ya CCBRT kupitia kitengo hiki ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na kuhakikisha Wanawake wote wanaopata huduma ya uzazi salama.
Hafla hiyo itakayofanyika Mei 7 mwaka huu katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Serikali wamekuwa wakitoa huduma ya Afya katika mifumo ya Afya ya uzazi kwenye mkoa wa Dar es Salaam, kujenga uwezo wa wataalamu wa Afya walioko kwenye vitengo vya Afya ya uzazi.
“Kitengo hiki kitafunguliwa rasmi mwezi Juni, tayali tumeanza kutoa huduma kwa Awamu tokea mwezi Januari na kufikia sasa tumezalisha akina mama wajawazito wapatao 37. Kitengo hiki kitatumika kama hospitali ya rufaa ya Kanda na tutakapoanza kutoa huduma kwa ukamimilifu wake tutakuwa na uwezo wa kuwahudumia akina mama wenyevujauzito hatarishi wapatao 12,000 kwa mwaka,” Alisema Bi Msangi.
Aidha katika hatua nyingine Bi. Brenda ametoa wito kwa wadau wote wa Afya ya uzazi kuwaunga mkono ili kuwezesha mazingira ya uzazi yaliyo salama, yenye staha na ubora kwa mama zetu na kwamba ifike Siku moja lila mwanamke aweze kutarajia ujauzito na kujifungua salama, Heshima na furaha.




