TAMASHA KUBWA LA UTAMADUNI AFRIKA KUFANYIKA ZANZIBAR MEI 23
CHAMA cha Waongoza Watalii Zanzibar (ZATO) kimeandaa tamasha la Utamadani la Afrika (FESTAC AFRICA) ambalo linalenga kukusanya na kuziunganisha nchi 54 za Afrika ili kuonyesha sanaa na utamaduni ambao unapatikana katika barani huko.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari ulifanyika katika hotel ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa ZATO Hassan Ally Mzee amesema lengo la tamasha hilo ni kuwakutanisha Waafrika na kujumuika pamoja ili kuweza kutangaza utamaduni wa Afrika kwa mataifa mengine.
Alisema mataifa mengi ya Afrika wanatarajia yatashiriki katika tamasha hilo ambapo kutakuwa na muziki wa bendi na kunatarajiwa kuwa na wazungumzaji wengi wakiwemo Marais wastaafu kama Jakaya Kikwete, Abeid Aman Karume, Mohammed Ally Shein, Rais mstaafu wa Botswana, Mabalozi na watu maarufu.
Aidha bw. Mzee ametoa wito kwa Waafrika kuhakikisha wanadumisha utamaduni na kulinda maeneo ya kihistoria kwa kuyatangaza kwenye vyombo vya habari.
Naye mwenyekiti wa maonyesho hayo Bw, Yinka Abioye amesema lengo la kuandaa tamasha lilikuwa ni kuona namna kuwaleta pamoja na kuwaunganisha waafika wote.
Hivyo wakaona waje na tamasha la kitamaduni kwasababu kila mwafrika ana utamaduni wake hivyo ni lazima watawaunganisha kwa pamoja na lengo kuu la tamasha hili ni kuunganisha Bara la Afrika.
Bw. Abioye ameyataja baadhi ya matukio ambayo yatafanyika katika tamasha hilo kuwa kutakuwa na Mkutano kubwa wa biashara lengo lake ni kukuza uelewa na mbinu za kibiashara za washiriki na kila mtu anakaribishwa kushiriki katika matukio yote.
Pia kutakuwa na maonyesho ya biashara na Makongamano yatakayoongozwa na watu mashuhuri wakiwemo maraisi wastaafu pamoja na michezo mbalimbali




