WAAJIRI WATAKIWA KUAJIRI MAAFISA UNUNUZI NA UGAVI WALISOAJILIWA NA PSPTB
Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Imetoa wito kwa waajiri nchini kuzingatia kujiri maofisa ununuzi na ugavi waliosajiliwa kwa lengo la kuongeza ufanisi na tija kwa taasisi zao.
Akizungumza jijini Dar es salaam, mkurugenzi mtendaji wa PSPTB, Bw Godfrey Mbanyi alisema kwa mujibu wa kifungu cha 11 kimeweka sharti la ulazima kwa kila anayefanya kazi za ununuzi na ugavi awe amesajilia na kuwa na taaluma hiyo.
"Napenda kuwakumbusha wakuu wa taasisi za umma na binafsi kuwa kwa mujibu wa sheria ya ununuzi na ugavi kumtaka kila anatefanya kazi hiyo kuwa mwana taaluma kuzingatiwa kwa lengo la kuongeza ufanisi katika taasisi zao" Alisema Bw. Mbanyi.
Alisema TSPTB imebaini bado kuna waajiri ambao mwekuwa wakikiuka sheria ya manunuzi na ugavi kwa kuajili wafanyakazi za ununuzi na ugavi ambao awana usajili wa TSPTB jambo ambalo ni kinyume na sheria na taratibu wa bodi.
Bw Mbanyi alibainisha kuwa kwa mujibu wa taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) pamoja na mamlaka ya kudhibiti ununuzi wa umma (PPRA) kuonyesha kuwa kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa sheria katika kitengo cha ununuzi kufatia kuwepo na wakuu wa ununuzi wa vitengo wasio na sifa za kitaaluma.
"Kumekuwepo na mapunyufu makubwa sana kwa mijibu wa taarifa ya CAG katika ukidhi wa sheria ya manunuzi wa umma na kanuni zake jambo linalopelekea serikali kuingia hasara"Alisema Bw. Mbanyi.
Bw. Mbanyi amechukua nafasi hii kuwataka wakuu wa taasisi kuhakikisha kuwa wataalam wote wanaofanya kazi katika kitengo cha ununuzi na ugavi wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma, miongozo, na kutoa huduma zinazokidhi viwango.
Aidha amewataka wanataaluma wa ununuzi na ugavi wa sekta binafsi na umma kufanya kazi kwa weledi na kutoa ushauri kwa umakini bila kuwa na hofu kwa lengo la kupata dhamani halisi ya fedha.




