Breaking News

KAMPUNI YA HERO MOTOCORP YATOA MSAADA WA PIKIPIKI TANO KWA JESHI LA POLISI

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akipokea nyaraka za makabidhiano ya Pikipiki tano kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya  Karemjee Jivanjee (KJL), Bw. William Kadiva.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwingelo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo akifafanua akiongea katika hafla ya kupokea msaada wa pikipiki tano kutoka kwa kampuni ya Hero Motocorp jijini Dar es salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ACP Jumanne Muliro akizungumza katika hafla ya kupokea msaada wa pikipiki tano kutoka kwa kampuni ya Hero Motocorp jijini Dar es salaam.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya  Karemjee Jivanjee (KJL) Bwana William Kadiva akiongea katika hafla ya kupokea msaada wa pikipiki tano kutoka kwa kampuni ya Hero Motocorp jijini Dar es salaam

Dar es salaam:
Jamii imetakuwa kuendekea kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapobaini kuwepo kwa viashiria vya uhalifu na uvunjifu wa amani zitakazo saidia jeshi hilo kuchukua hatua dhabiti za kuzuia matukio hayo 

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwingelo mara baada ya kupokea msaada wa Pikipiki Tano aina ya Hunter 125cc kutoka kwa Kampuni tanzu ya Karemjee Jivaniee Ltd( KJL),

Mhe Mwingelo amesema msaada huo  umekuja wakati sahihi kwani utasaidia kuongeza ufanisi zaidi katika utendaji wa majukumu yake hususani kupambana na vitendo vya uhalifu 

"Msaada huu umekuja muda muafaka kwani utaliwezesha jeshi la polisi kutekeleza kwa ufanisi kuzuia na kupambana na vitendo vya uhalifu" Alisema Mhe. Jokate

Alisema pikipiki hizo zitasaidia kuongeza doria kuongeza ulinzi na usalama kwa Wananchi waweze Kufanya kazi Katika maeneo yao wakiwa salama kwa kukomesha vitendo vya uhalifu hususani wizi wakutumia Pikipiki wa kukwapua maarufu Kama Vishandu.

Mhe Jokate ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo aliongeza kuwa  mapambano dhidi ya uhalifu ni jukumu letu sote jamii iendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za uhalifu na hata Kama ni ndugu yake.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ACP Jumanne Muliro amesema hatua iliyofanywa na Kamati ya Ulinzi na Usalama kutafuta  suluhu ya masuala ya Usalama ni jambo la kupongezwa na kuzitaka kanda zingine za kipolisi ikiwemo Kanda ya Polisi Kinondoni na Ilala kuiga Mfano huo.

"Napenda kuwatahadhalisha askari mtakaotumia pikipiki hizi,msitumie kwa kuomba rushwa, msizitumie kwa ajili ya kuwasumbua Wananchi, msizitumie kwa kusindikiza wahalifu, hivyo zitumike kwa kazi moja tu ya kuleta suluhu ya uharifu kwa Wananchi " Alisema Kamanda Muliro.

Nae Meneja Mkuu wa Kampuni ya  Karemjee Jivanjee (KJL) Bwana William Kadiva amesema wametoa msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa lengo la kuboresha utendaji wa jeshi hilo kutokana na kuwa bora na zenye uwezo wa kusafiri mpaka umbali wa kilometa 60 hadi 70 kwa kutumia mafuta kidogo ambayo ni lita moja.