TAASISI YA PINK TIE YAZINDUA KAMPENI YA KUSAIDIA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI
Katika kuhakikisha tatizo la watoto wa mitaani linakomeshwa, Serikali imesema haitosita kuwachukulia hatua wazazi au walezi watakao bainika kuwasafirisha watoto kutoka vijijini kuja mjini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Kataa Mitaani ya Pink Tie Foundation, Mkuu wa wilaya ya Ilala, mheshimiwa Bwilaguzu Lubigija amesema serikali tayali imeshaandaa maeneo maalum ya kuwaweka ili kuondokana changamoto za watoto mitaani.
"Na wale wenye ujuzi watapewa nafasi ya kufanyakazi kulingana na ujuzi wao katika baadhi ya taasisi". Alisema Bwilaguzu.
Mhe. Lubigija alisema kumekuwepo na changamoto kubwa ya watoto kuchukuliwa vijiji kuletwa mjini kwa ahadi au kurubuniwa kuwa wanakuja kupatiwa kazi matokeo yake mambo yanakuwa tofauti hivyo kuishia kuwa watoto wa mtaani.
Naye Mwenyekiti wa Pink foundation Bi. Salma Dakota alisema lengo la kuanzishwa kwa kampeni ya He/She ni kusaidia kupunguza au kuondoa tatizo la watoto wa mitaani.
"Kampeni hii imeanza rasmi 6 ambapo itaitimishwa tarehe 16 mwezi Juni ikiwa na lengo la kuwakutanisha pamoja na kuona namna ambavyo wanaweza kulimaliza tatizo hilo la watoto wa wanaoishi katika mazingira magumu" Alisema Bi. Dakota.








