Breaking News

RC MAKALLA: MAONYESHO YA 46 YA SABASABA 2022 YAMEFANA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Sera nzuri na mwelekeo Bora alioonyesha Rais Samia Suluhu Hassan kuitangaza Nchi kimataifa hususani Royal tour vimechagiza Maonyesho ya 46 ya sabasaba kuwa na mwamko mkubwa na ushiriki wa Makampuni mengi kutoka ndani na nje ya Nchi.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea Maonyesho hayo ambapo amefurahi kuona zaidi ya Nchi 22 zikishiriki Maonyesho hayo na Kampuni za 3,200 za Ndani 180 kutoka nje ya Nchi.

- Zaidi ya Mataifa 22 yameshiriki, Kampuni za ndani 3,200 na Kampuni 180 kutoka nje ya Nchi.

- Asema Sera nzuri na mwelekeo wa Rais Samia kutangaza Taifa imevuta Makampuni mengi ya nje ya Nchi kushiriki.

- Awapongeza TANTRADE kwa uratibu na kurudisha hadhi ya Maonyesho hayo.

Aidha RC Makalla ameipongeza Tan trade kwa kuratibu vizuri Maonyesho hayo na kutoa wito kwa Wananchi kutembelea Maonyesho hayo ili kujionea uharibifu na bidhaa mbalimbali

Pamoja na hayo RC Makalla amepongeza pia ubunifu wa kuanzisha route za Usafiri wa Mabasi ya mwendokasi mapaka kwenye Viwanja hivyo jambo linalorahisisha huduma ya usafiri.