Breaking News

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA KUJA KIVINGINE

Posta Masta Mkuu Makris Mbondo akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam:
Shirika la Posta Tanzania imeboresha huduma zake za usafirishaji na kuja na huduma mpya za utumaji wa fedha bima, kukata tiketi ya ndege pamoja na biashara mtandao.

Hayo yamebainisha na Posta Masta Mkuu, Bwana Makris Mbondo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mbodo amesema shirika la Posta limekuja kitofauti na wananchi wafikee katika banda lao waweze kupata maelezo zaidi kuhusiana na huduma zao mpya.

"Huduma zetu zote zinapatikana hapa ikiwepo huduma mpya tulizozianzisha tunaonyesha namna tulivyoboresha huduma zetu za usafirishaji sasa mwananchi anaweza kupata msg ya mzigo wake kupitia namba zake za simu, ataweza kupata maelekezo kupitia simu yake tangu mzigo unaondoka mpaka kufika na kupitia anauni ya makazi tunasafirishia mpaka nyumbani kupitia anuani ya makazi aliyonayo mteja" Alisema Mbodo

"Posta sisi ni mawakala wa taasisi mbalimbali, tumeingia makubaliano kutoa huduma na taasisi nyingi kutokana na mtandao wetu ulioenea ndani na nje ya nchi tuna ofisi zaidi ya 350 ndani ya nchi, na ofisi zaidi ya 670,000 kote duniani, ukitaka kutumia huduma za kibenki unatuma kupitia ofisi ya posta mzigo wako unakua salama" Alisema Mbodo

Pia Shirika la Posta kwa sasa wanahuduma za bima na tayari wameingia ubia na wakala na kampuni ya ndege ya Tanzania kwa ajili ya kukata tiketi za safari za ndani ya nchi na nje ya nchi.

Shirika la Posta inasajili biashara mtandao huduma hii inapatikana kwa lugha zote duniani Posta inachofanya ni kusafirisha mzigo popote duniani




Posta Masta Mkuu Makris Mbondo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Posta ndani ya banda lao kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.