ADC YAENDESHA MAFUNZO KWA WANACHAMA WAKE JUU YA UMUHIMU WA USHIRKI WA SENSA
Mwenyekiti wa ADC Hamad Rashidi akizungumza katika katika mkutano huo makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam
Katibu mkuu wa chama cha ADC DOYO HASSAN DOYO akifafanua jambo katika mkutano huo
Katibu mkuu umoja wa Wanawake ADC. Bi zuwena Mohamed akiongea na wanachama wa chama hicho walioudhulia mkutano huo uliofanyika makao makuu ya chama jijini Dar es Salaam.
Dar es Salam:
Chama cha ALLIANCE for Democratic change (ADC) kimewataka wanachama wake na wananchi kwa ujumla kujitoka kuhesabiwa katika zoezi sensa Agost 23 mwaka huu na kuondoa dhana za kizamani kuwa kuhesabiwa ni mikosi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya ulimishaji wananchi kuhusu umuhimu wa sensa Mwenyekiti wa ADC, Hamad Rashidi amesema ili nchi iweze kujiendesha na kupanaga mipango ya maendeleo vizuri ni lazima kuwe na takwimu sahihi za watu makazi yao.
Aidha amesema kuwa ADC katika kila jambo la kitaifa itaendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha swala hilo linakwenda vema kama lilivyopangwa bila kujali tofauti za kisiasa baina yao na utawala uliopo.
Nae katibu mkuu wa ADC DOYO HASSAN DOYO amesema ADC imeandaa mpango maalumu wa nchi nzima wa kufanya warsha na uhamasishaji wananchi kujitokeza kuhesabiwa hapo Agost 23.
"Lengo la mkutano huu ni kuamasisha wanachama na wafuasi kutambua umuhimu wa kushiriki katika sensa ya watu na makazi kwa maendeleo ya taifa" Alisema Bw. Doyo
Kwa upande wake Katibu mkuu umoja wa Wanawake ADC bi zuwena Mohamed amesema sensa ta mwaka huu sio ya kwanza kufanyika na lengo lake ni kujua idadi ya watu kwaajili ya kupanga maendeleo yao hivyo ni vema kila mwanachi akajitokeza kuhesabiwa na kuzingatia kutowaficha watu wenye mahitaji maalumu na changamoto mbalimbali ikiwemo ulemavu







