MASHAKA NGOLE ACHUKUA FOMU KUWANIA KUTEULIWA NA CUF KUWA MGOMBEA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI
Naibu Mkurugenzi mipango na chaguzi CUF taifa. Bwana Yusuph Mbungiro akimkabidhi fomu Wanasheria mwanandimizi wa Chama cha wananchi CUF Bwana Mashaka Ngole leo 3 augost makao makuu ya chama hicho buguruni jijini Dar es salaam
Wanasheria mwanandimizi wa Chama cha wananchi CUF Bwana Mashaka Ngole akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho buguruni jijini Dar es salaam mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kutaka kuteuliwa na chama hicho kuwa mgombea wa bunge la afrika mashariki.
Naibu Mkurugenzi mipango na chaguzi CUF taifa. Bwana Yusuph Mbungiro akifafanua jambo kwa waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho buguruni jijini Dar es salaam
Dar es Salaam:
Wanasheria mwanandimizi wa Chama cha wananchi CUF Bwana Mashaka Ngole leo tarehe 3 August amechukua fomu rasmi ya kuomba chama hicho kumpitisha kuwa mmoja ya wagombea watakao wakilisha chama katika uchaguzi wa wabunge wa bunge la afrika ya mashariki.
Akuzngumza mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo makao makuu ya chama hicho buguruni jijini Dar es salaam amesema amefikia uamuzi wa kuchukua fomu ya kuomba chama kumteua kukiwakilisha kama mgombea wake kwani anao uzoefu wa kutosha kuweza kukiwakilisha chama na taifa kwa ujumla.
"Nimejitokeza leo kuchukua fomu ya kuomba chama changu kunipitisha kukiwakilisha kuwa mgombea katika bunge la afrika mashariki kwani vigezo ninavyo na naweza kuiwakilisha taifa katika chombo hicho" Alisema Mashaka.
Mapema akimkabidhi fomu ya kuwania nafasi hiyo Naibu Mkurugenzi mipango na chaguzi CUF taifa Bwana Yusuph Mbungiro amesema mgombea amekidhi vigezo hivyo kumpatia fomu kuweza kuomba chama hicho kumpitisha kuwa mgombea wake.
"Nimepitia vielelezo na vigezo vyote na kuona vimekamilika kwa mujibu wa katiba ya chama hivyo tunampatia fomu ambayo anatakiwa kujaza na kuirejesha kabla ya tarehe 15 August mwaka huu" Alisema.
Alisema tangu kuanza rasmi kwa zoezi la kutoa fomu tarehe 27 julai mwaka huu tayali jumla ya wagombea sita wameshajitokeza kuchukua fomu kuwania kuteuliwa na chama hicho kukiwakilisha katika uchaguzi wa bunge la afrika mashariki.
Bw aliongeza kuwa wagombea wote wanatakiwa kurudisha fomu kabla ya tarehe 15 August baada ya tarehe hiyo wataruhusiwa rasmi kuanza kujinadi kwa wanachama ili kuweza kuomba kura wakati wakingoja kutangaziwa rasmi tarehe rasmi ya kikao cha baraza kuu la uongozi taifa.
"Kuanzia terehe 15 mwezi huu wagombea wote wataanza kufanya kampeni za kuomba kura kwa wanachama katika kipindi chote mpaka itakapo tangazwa tarehe ya kikao baraza kuu la uongozi taifa ambapo utafanyika mchujo kupata washiriki watakao wakilisha chama hicho kugombea katika bunge la afrika ya mashariki"






