Breaking News

"BOXING WITH TOURISM" DULLAH MBABE KUZICHAPA NA ERICK KATOMPA JIJINI ARUSHA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lady in Red Promotion Sophia Promotion, Bi Mwakagenda akiongea na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya kuelekea pambano la Dullah Mbabe na Erick Katompa litakalofanyika Novemba 25, 2023 jijini Arusha.

Dar es salaam
Bondia machachali nchini Dullah Mbabe atapanda ulingoni kuzichapa na bondia Erick Katompa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo)  Novemba 25 jijini Arusha.

Akizungumzia maandalizi kuelekea pambano hili Mkurugenzi wa Kampuni ya Lady in Red Promotion, Bi Sophia Mwakagenda amesema maandalizi yote kuelekea pambano hilo lilobeba kauli mbiu ya “Boxng with Tourism” yamekamilika na mabondia wote wamethibitisha kushiriki pambano hilo.

“Tupo hapa kusainiana mkataba Kati ya Dullah Mbabe na Katompa kwa ajili ya Pambano hilo lenye lengo la kuunga mkono kuhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kukuza Utalii nchini,” Alisema Bi. Mwakagenda.

Alisema Pambano hilo la raundi 10 na litaambatana na mapambano zaidi ya 10 ya utangulizi kutoka kwa mabondia mbalimbali wakali hapa nchini kuonyeshana umwamba.

Aidha bi. Mwakagenda aliongeza kuwa Pambano hilo ambalo lengo lake kubwa ni kuutangaza Utalii, anaamini kupitia mabondia hawa watafanikiwa kuutangaza utalii. hivyo amewataka mabondia hususani wa Tanzania kutambua kuwa wanao wajibu wa kuutangaza Utalii wa nchi yao.

Kwa upande wake Bondia Dullah Mbabe amesema amejiandaa vizuri kuelekea Pambano hilo ili kulipiza kisasi kwani Pambano lao la kwanza alipigwa.

Nao uongozi wa Chama cha Ngumi Tanzania (TPBRC) umesema kwamba utahakikisha Pambano hilo linafanikiwa. Hivyo umemhakikishia ushirikiano promota wa pambano hilo.