Breaking News

PROF. LIPUMBA ALAANI KITENDO CHA POLISI KUVAMIA NA KUZUIA MKUTANO WAO JIJINI DAR

Mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akifafanua katika mkutano wake na waandshi wa habari kuhusu kitendo cha jeshi la polisi buguruni kuvamia na kusitisha mkutano wao wa hadhara siku ya tarehe 24 November 2023 makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa chama cha CUF ilala, bwana Hamis Chambuso alielezea kilichotokea siku ya tarehe 24 November 2023 kufatia tukio la jeshi la polisi buguruni kuvamia na kusitisha mkutano wao wa hadhara siku ya tarehe 24 November 2023 makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam. 

Dar es salaam
Chama cha wananchi CUF kimelaani kitendo cha jeshi la Polisi kuvamia na kuvunja mkutano wao uliokuwa ufanyike buguruni na kukata vingozi na wanachama wa chama hicho siku jumamosi ya tarehe 24 November 2023.

Alizungumza makao makuu ya chama hicho buguruni Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba amesema kitendo hicho cha jeshi la polisi buguruni si cha kiungwana licha ya wao kufuata taratibu zote zinazotakiwa kisheria na kupatiwa kibali cha kufanya mkutano huo. 

Alisema katika kadhia hiyo jumla ya viongozi na wanachama saba wa chama hicho waliokamatwa licha ya jitihada za viongozi kuchukua hatua za mapema kwa kufika kituo cha polisi buguruni kwa lengo la kuonana na OCD wa kituo kupata ufafanuzi na kuwawekea dhamana viongozi na wanachama wa chama hicho walioshikiliwa kituoni hapo alionyesha kutoonyesha ushirikiano na akiwajibu kwa jeuri.

"Mara baada ya kadhia hiyo viongozi walifika kituo cha polisi buguruni kwa lengo la kuonana na OCD ili kupatiwa ufafanuzi pamoja na kuwawekea dhamana viongozi na wananchama waliokamatwa OCD hakuonyesha ushirikiano kwa viongozi hao" Alisema Prof. Lipumba 

Alisema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia ilishafanya jitihada za kurejesha maridhiano lakini kwa jambo hilo kuzolotesha jitihada za mhe rais za kuleta maridhiano hivyo serikali kutambua kwamba huku chini kuna watu wenye mpango wa kuzuia falsafa ya maridhiano ya kisiasa yaliyofanywa na Rais.

Alisema jeshi la polisi lisiturudishe kwenye siasa ya mapambano basi sisi tunataka siasa za kujenga hoja na maridhiano ambazo hata Rais Samia mwenyewe anatangaza siasa za maridhiano, kufatia tumio hili inaonyesha kuwa bado falsafa ya mhe rais juu ya maridhiano bado aijaeleweka kwa baadhi hivyo nishauri serikali iandae utaratibu wa kutoa mafunzo kuelezea siasa za maridhiano ni nini. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha CUF ilala, bwana Hamis Chambuso amemtaka waziri wa mambo ya ndani kuomba rai mara moja kufatia kitendo kilichofanywa na OCD wa Buguruni licha ya chama kufuata taratibu zote wakati maandalizi siku ya mkutano Polisi wakavamia na kuvunja mkutano huo.

“Kitendo hiki ni cha kukemewa kwa Tunajipanga kwenda kwenye uchaguzi hivyo vitendo kama hivi havikubaliki ukizingatia tupo Dar es Salaam palipofanyika maridhiano sasa sijui huko mikoani kutakuwaje?”Alisema Chambuso.